Tofauti kati ya Bachelor degree itolewayo University na Institutes ni ipi?

Balokola

Senior Member
May 9, 2014
133
90
Hapa nafkr wengi nona na mnasikia kuhusu Bachelor degree
Mimi nataka kufahamu,je ni kipi kinacho tofautisha kati ya mtu anayesoma IFM na UDSM mfano Bachelor in Economics?
Au Tofauti ya anayesoma engineering degree ATC,DIT na MUST na yule anayesoma St Augustine,UDSM,UDOM na SUA?
 
Ukitaka linganisha kwa kozi. Mtu aliyesoma Bachelor of Economics na aliyesoma Bachelor katika Engineering wanatofautiana kitaaluma hata kama wamesoma chuo kimoja.
 
mtoa mada ulichouliza ni sawa na kuuliza nini tofauti kati ya Institute na University.
Ngoja tusubiri majibu.
 
Hakuna tofauti. Labda nikupe tofauti ya institute, college na universty.
1: Hapa hutolewa elimu ya ujuzi tu. Institute inaweza kuwa chini ya taasisi nyingine ya elimu ya juu au chini ya Universty. Elimu ya ujuzi tu kwa maana gani? Kwa mfano, ukisoma bachelor degree yoyote chuo kikuu hapa Tanzania lazima kutakuwa na course za Development Studies na Communication Skills. Lakini kwenye institute unaweza usikute kitu kama hicho.
2:College, hapa hotolewa elimu iliyoegemea upande mmoja tu, kwa mfano biashara au uhandisi.
3:University inakuwa na college au faculty zenye kutoa elimu mbalimbali. Kwa mfano, biashara, sheria, uhandisi, ualimu n.k

NB: Kwenye institute pia unaweza kuta kunatolewa fani mbalimbali lakini ni elimu iliyoegemea ujuzi tu.
 
ukwel mtupu huu ,shukran sana
 
Back
Top Bottom