Tofauti kati ya Assets and liabilities

Dullah Ally

Member
Mar 24, 2019
16
12
Umasikini sio kitu kizuri naimani hakuna anaependa kuwa masikini kila mja anapenda kuwa na maisha mazuri but usikubali kuwa masikini kifikra sababu kuwa hivo ni kujichelewesha katika kufikia malengo yako. Mafanikio huchangiwa na mambo mengi mojawapo likiwa ni watu wanaotuzunguka wanasaidia sana katika safari zetu kuyaendea mafanikio, marafiki..
Pia watu tuliowengi hatuishi kwenye ndoto zetu mfano ndoto yako ilikuwa kuja kuwa daktari, but hivi sasa wewe ni mwalimu upo pale sio kwaajili ni pasion yako kuwa mwalimu but umekuwa mwalimu kwakuwa you have no way.. So sidhani kama utakuwa na mapenzi na hiyo kazi na matokeo yake you will work for money na ndugu zangu nawaambia ukiruhusu emotions zikuendeshe basi utafanya kazi kwaajili ya kupata pesa na utaamini kuwa pesa ndo kila kitu, na utaamini pesa zinamaliza matatizo.
  1. Lakini sio kweli kama pesa inamaliza matatizo wapo waliokuwa wanapata mshahara wa dollar100 na walilia shida na kila siku kauli zao zilikuwa nikiongezewa mshahara nitafanya vizuri bahati nzuri ikatokea bahati mshahara upande ufike dollar500 na bado watasikika wakisema nikiongezewa nitafanya vizuri zaidi wanasahau kuwa cash flow inapokuwa kubwa hata bills zinaongezeka na tunasahau kuwa na assets ni muhimu zaidi kuliko kuwa na liabilities katika kitabu cha RICH DAD POOR DAD kinaelezea vizuri sana kuhusu Assets and liabilities ipo hivi assets inaleta pesa mfukoni while liability hutoa pesa mfukoni wengi wetu tunaamini kuwa House ni asset but sio kweli na hicho ndicho tunakosea ili ku overcome haya yote lazima tujiwekee asset zaidi kuliko kuwa na liability nyingi unakuta mtu ndo kaanza kazi tuu mara kachukua mkopo wa Gari, hilo gari sasa haliwezi kuwa asset utahitaji kuweka mafuta, services so badala ya pesa kuja mfukoni matokeo yake pesa inaondoka mfukoni otherwise labda iwe gari ya biashara but kama ni ya matembezi ndugu yangu ni janga hilo watanzania wengi tunahisi Gari na nyumba ndo maisha umeyaweza may be kama hauna ndoto kila siku lazima uwe na next plan baada ya nyumba na gari what is next... Samahanini kama nimewakwaza nimejaribu kuwasilisha nilichonacho
 
Mkuu umetoa maelezo mengi bila kuhitimisha unalenga nini? Licha ya pale ulipoandika kuna tofauti kati ya liability na asset.

Labda kwa kujazia , nafikiri unataka kumaanisha kwa nini watu wanakuwa maskini na wengine wanakuwa matajiri.

Moja wapo ni kuweza kujua kanuni za kifedha au ujuzi wa kifedha ( financial intelligence).

Wakati maskini na mtu kati ( middle class ) analimbikiza liability ( mfano nyumba ya kuishi, TV inch 55 na kuendelea, magari ya anasa na vingi kama hivyo), upande mwingine kuna yule anamiliki asset ( vitu ambavyo vinaleta mapato ) anafungua biashara, anajenga nyumba ya biashara, ananunua viwanja nk nk.

Hivyo anaendelea kukusanya really asset anakuwa tajiri. Yule anayekusanya liabilities akifikri anamiliki asset, mwishowe huwa anajikuta yupo hohehahe...
 
Asset ni kitu kinacho kuingizia pesa, liability ni kitu kinachitumia pesa zako.
Unaweza ukawa na rafiki asset au rafiki liability
Unaweza ukawa na simu asset au simu liability
Unaweza ukawa na nyumba asset au nyumba liability.
Kwa kifupi. Kila kitu kinaweza kuwa asset au liability. Inategemea na jinsi unavokitumia. Unakitumia kuzalisha pesa au kutumia pesa?

Watu wanakuwa maskini kulingana na jinsi wanavyotumia pesa (how they spend their money). Ukitumia pesa kununua asset unajijengea uwezo wa kifedha (building financial stability) na unakuwa na nafasi kubwa ya kuwa tajiri. Ukiitumia kununua liabilities ndo unajijengea umaskini.
Anyways, mambo ni mengi
 
Back
Top Bottom