habari wadau jamii forums,huku ninakoishi kumezuka mtindo fulani katika lengo la kutaka kufyatua tofali nyingi kwa kutumia mifuko michache saruji ,watu wameanzisha utaratibu wa kuchanganya cement na chokaa ili mfuko mmoja badala ya kutoa tofali 40/45 sasa unatoa tofali 60 mpaka 70. Swali langu kwenu wataalam wa mambo haya ya ujenzi,hivi kuna uhusiano wowote kati hivi vitu(cement na chokaa), na je uhusiano huo ni wa tija kama jinsi ambavyo hao ndugu zangu wamekuwa wakiamini(yaani tofali zitokanazo na huo mchanganyiko ni zinadumu?)
Naomba ufafanuzi kwa mwenye ufahamu wa hilo suala