Nilianzisha hii Kitambo sana.
Amani iwe kwenu.
Nilikuwa napitia maandiko na kuna sehemu imenivutia na kuamua ku-share pamoja na waaminio katika hili.
Nimeileta mada hii chit chat kwa ajili ya watu wa hapa na si kule jukwaa la dini maana si wengi tunapita huko. Mods 'mnisamehe (source-Mr. Ebo)
Baada ya hayo naomba nianze na mada hii inayohusu ishara na imani.
Ninavyoona mimi sasa hivi waamini tumekuwa tukihama kutoka pointi A kwenda pointi B tukimsaka Yeye aliye Kweli kwa kufuata ishara zinatolewa na wahudumu wa sehemu hizo. Hii ikanifanya nitamani kujua ni kipi kilicho muhimu zaidi katika maisha ya MKRISTO? Ni ishara au imani?
Nimeona katika agano la kale Mungu aliwaagiza manabii kutumia ishara ili watu wapate kuamini kuwa wametumwa na Mungu wa Ibrahimu.
mfano hapa naupata Kutoka 4: 1-9, unaelezea majibizano kati ya Musa na Mungu alipomtokea kumpa ujumbe wa kuwaokoa waisrael.
Hapa uwezo aliopewa Musa wa kufanya miujiza ilikuwa kwa ajili ya kuwafanya waisrael waamini kuwa ametumwa na Mungu na kweli alimtokea.
Katika Agano Jipya kitabu kilichoongelea zaidi mada hii ni Injili ya Yohane.
katika Agano Jipya, nimejifunza kwamba Yesu alikuwa anatumia ISHARA(miujiza) kwa ajili ya kuvuta watu (kumbuka kipindi hicho hakukuwa na makanisa ya yeye kufundishia zaidi ya masinagogi ya wayahudi ambao hawakuvutiwa naye) ili aweze kuwafundisha neno au baada ya kufundisha neno alitoa ishara ili wapate kuamini.
Mfano nimepitia Yohane4: 48-50 na 53- 54, hapa tunamwona afisa/diwani aliyekuwa na bintiye mgonjwa huko Kapernaumu. Anamfuata Yesu aende kumponya bintiye, lakini Yesu anamwambia aende tu bintiye amepona. Baada ya yule ofisa kuamini tu bintiye alipona wakati ule ule.
Muujiza huu ulifanya afisa huyu na familia yake ipate kuamini kwamba Yeye ndiye.
Katika Yoahne 6: 9-11 na 14
Hapa nimezidi kuona Yesu alivyotumia ishara ili watu wapate kumwamini. Kisa hiki kinahusu Yesu kuwalisha watu elfu tano kwa mikate 5 na samaki 2, baada ya wale watu kushiba wakaamini.
Katika Yohane 6: 26-27, naomba ninukuu
' Yesu akawajibu akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanifuata, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani Mungu.'
maneno haya yanaonesha kuwa tunapochagua kufuata neno la Mungu iwe zaidi ya matamanio yetu ya duniani kama chakula, mali, afya na vingine vingi maana ule uzima wa milele ndio linatakiwa kuwa tamanio letu la kweli.
Sasa hii hangaika tunayoifanya sasa hivi kwa ajili ya vitu vya kidunia, tujikumbushe na kama tunaona tumeacha lengo kuu la Yesu mwenyewe tujirudi na kufuata iliyo kweli.
Katika Yohane 11: 14-15
Hiini kisa kinachohusu kufufuliwa kwa Lazaro, ishara hii ilisaidia pia walioshuhudia kuamini.
Baada ya Yesu kufa na kufufuka, nimeona msisitizo wa kuamini unabadilika kutoka kwenye kuamini kwa kuona ishara na kuamini kwa kuwa umeyasikia mafundisho ya Yesu na kuamini. Na hii kwa mtazamo wangu inakuja kwa sababu sasa hivi tayari kanisa tunalo ambalo ni Yesu Kristo mwenyewe tofauti na awali ilibidi afundishe kwa ishara kuvuta watu na kuwafanya waamini. Yesu mwenyewe ndie muujiza mkuu kuliko yote, na kikubwa anachoangalia kwetu ni nafsi zetu za ndani na imani yetu thabiti kwake na si kingine.
Katika Yohane 20: 24-29
Kisa hiki kinahusu Yesu alipowatokea mitume wake, lakini Tomaso hakuwepo na hakuamini.
Yesu akasema '.... Heri yao wale ambao hawajaona, lakini wameamini'
Kuanzia hapa naona Yesu anatuasa tuamini bila kutafuta ishara za kidunia. Kuna kilicho kikuu kuliko ishara hizi tunazozitafuta sasa.
Katika Mathayo 12: 38-42 na Mathayo 16:1-4
Hapa naona akiwakemea wafarisay waliokuwa wakitaka afanye ishara, tena kwa maneno makali sana, naomba kunukuu kidogo tu '... Kizazi hiki kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona...'
Hapa naona anaongelea ishara kuu ilikuwa kifo na ufufuko wake.
Baada ya kuandika haya, naomba kama waamini tujiulize, je tunaenda makanisani kutafuta ishara au kweli ambayo ni Yesu Kristu mwenywe?
Je mahitaji yetu ya kibinadamu yameleta upofu mioyoni mwetu hata tunashindwa kuitafuta kweli na kutafuta ishara?
Kila mtu ana majibu yake kulingana na anachofahamu. Lakini wito wangu kwa waamini wa sasa ni kurudi katika misahafu yetu na kuitafuta kweli hii.
Maana tunaambiwa siku za mwisho ni wengi watakuja kwa jina lake lakini hawatakua wake.
Basi tutafakari haya wakati tunajiandaa kwa ajili ya kesho kwenda kuabudu.
Nawatakia siku njema na karibu kwa kuchangia mada hii ili tuendelee kukumbushana vitu muhimu katika kujiandalia makazi ya milele.
Mbarikiwe sana!
Sina access na jukwaa hilo, na sijaomba na bado sina uhakika kama nataka kuingia au la.
Any way; yote sawa, wana heri sana watu kama ninyi lakini sisi ambao imani yetu hushake once in a while tunahitaji kitu cha ziada.