Kwanini walalamika wakati macho unayo..
Eti wataka julishwa wakati simu kimeo...
Ungekua umestaafu ungeshakosa mafao..
Kloro endelea tuone yako mazao!
Tena hakuonekana, bundi ulipogundua
Ukweli hakuukana, kusepa aliamua
Kijana matata sana, gwiji limekukimbia
Watu wanaulizana , fani ameisusia?
Nauliza klorokwini, Jibu hutaki nipea,
kwako nimekosa nini, hutaki kuniambia?
Siredi liko jamvini, ODM sijajua?
Kwanini hukunambia, kuna sredi umerusha.
Unajua yangu fani, ni kama ya kwako pia,
Tunapoingia vitani, Utengano twachelea,
Leo imekuwa gani, umesusa kunambia?
Kwanini hukunambia, kuna sredi umerusha?
Nilijua utakuja, hilo sikulichelea
Nilihofu kujafuja, ratiba za kutibia
Wagonjwa wetu wamoja, shifti nazitambua
Na sasa weka mirija, ya maneno kuchambua.
Sasa hivi nitatoka, nawahi kwenye tukio
Lizzy nampa mkeka, ayajibu usemayo
Umtibu akitaka , mrembo sio mchoyo
Rekodi utaziweka, dozi ulotoa leo
Swali lake klorokwini, Kwanini wamjibia?
Pilipili i shambani, yanini yakuwashia?
Ntakufukuza nyumbani, ujukuu kuuvua.
Siku tena kirudia, nitakuchapa bakora!
Kaniruhusu mwenyewe maswali kumjibia..
Hata yakiwa ya wewe babu wa kusingiziwa..
Bila haya wanitisha nyumbani kunitimua..
Unadhani sina ujanja pa kwenda sijaamua!
aaah! mods naomba mic niwakilishe.
oh! baby!
nimekaa na kutulia, mengi nimefikiria
Mawazo yamenijia, tangu tulipoanzia
shairi nakutungia , nielewe my dia
mwenzio ninaumia, please say wewe pia
Kila nikikuangalia, kweli umekamilika
nguvu zinaniishia, nikuite malaika?
moyoni ninaumia, mwenzio nasononeka
Penzi lako nalilia, usije wakakuteka
Natamani kuwa nawe, sekunde kila dakika
Liwalo acha na liwe, moyoni nimekuweka
Mola acha asifiwe, alokuumba ukaumbika
Daima mimi na wewe, wazi wazi natamka
Napenda sauti yako, ukitaja jina langu
Hufichi hisia zako, ukiwa pembeni yangu
Kukusaliti ni mwiko, umetosha kiu yangu
Milele mimi ni wako, kwavile wewe ni wangu.
Nasifu zako tabia, Wazazi nawapa sifa
Mtoto umetulia, akili na maarifa
"Honey! nimekupikia", unanipa taarifa
Darling nimekuzimia, nakupa zote nyadhifa.
Usiku ukiingia, mapema wajitayarisha
Visa wanisimulia, vyengine vya kuchekesha
Uchokozi waishia, na kuanzisha tamasha
Nami nalimalizia, na koja nimekuvisha.
Macho ukiniangalia , taabani sijiwezi
mwendo u kitembea, laniuwa lako pozi
Nyumbani nakungojea, fanya hima laazizi
Zawadi mekuletea , za kukupa usingizi.
Nina mengi ya kusema, lakini muda hautoshi
Nakuombea uzima, Uzidi wako ucheshi
Unithamini daima, kwa harusi na mazishi
Ewe changu chema, Unukiae marashi.
Ni malenga wenu klorokwini a.k.a ileile "bukta la jeshi"
Ni vipi nimekimbia, uzushi mwanizushia
vina vimenishia, hayo mwahadithia
jamvini narudia, kama ilivyo sheria
Majukumu yamebana, na huku niliko pia
heheh wale ni ndugu zetu wa kufikia, wao walikuwa wanaishi karibu na bunge, sasa wamekuwa wanasiasa, sisi tulihamia karibu na Bakita ndo tumeishia kutunga mashairi ya mchiriku. hehehHivi klrokwini na asprin wale ndugu zenu wengine Quinine na vancomycin vp wao ktk fani, maana najua nyie dugu moja
heheh wale ni ndugu zetu wa kufikia, wao walikuwa wanaishi karibu na bunge, sasa wamekuwa wanasiasa, sisi tulihamia karibu na Bakita ndo tumeishia kutunga mashairi ya mchiriku. heheh
Mantiki hapa ni kwamba unaweza ukaandikiwa kwenye same prescription dozi ya klorokwini na aspirin lakini milele hauwezi kupewa dozi ya klorokwini na quinine at the same time, Hivyo quinine akitibu wanasiasa klorokwini inabidi atibu MMU.Nilikuwa nafikiri wewe na Qunine ndo tumbo moja maana wote ni anti malaria, hivi huyu Asprin ndugu zake si wakina non steroid anti inflamatory drug au nimekosea?
</p>Mantiki hapa ni kwamba unaweza ukaandikiwa kwenye same prescription dozi ya klorokwini na aspirin lakini milele hauwezi kupewa dozi ya klorokwini na quinine at the same time, Hivyo quinine akitibu wanasiasa klorokwini inabidi atibu MMU.
Yakuonea ni vipi?, mbona unajishukia?
Mwanakijiji yuwapi?, ndio twamuulizia
Nikueleze kwa ufupi, nini kilichotokea
Yeye alikuja na yepi?, ndege alimtungua
Kiranja aspirini , akamuhoji malenga
Aliuliza hadharani, laivu bila ya chenga
Ndege huyu ndege gani?, aliuliza wahenga
Si bundi jama lakini?, malenga kapiga chenga
Tokea zama za hapo, Wa kijiji kapotea
Ndio leo hapa tupo, stori twakumbushia
Uzushi kwako haupo, mwengine twaongelea
Itulize roho yako, mistari endelea
ushairi wetu!!
Safi sana mjukuu wa Shaaban Robert
Hapo nimekusikia, na sasa tuko pamoja
Bango tutawashikia, tutaunnda na sinema
Lizzy atasaidia , CPU keshakusoma
Mbu namuaminia, Asha D hayuko nyuma
Jeshi kamili tunalo, hapa hapa Jeiefu
Afrodenzi asemalo, lasikika kwa maelfu
MJ1 kwa midahalo, mjukuu mtiifu
Aspirin my fello , hoja zake ni nadhifu
The Finest wa mbagala, wengi wanamuheshimu
Uporoto hajalala , punde atatia timu
Michelle zake makala, amri utasalimu
Wiselady mpenda mola, achukiae mizimu
Tuna miss wa mpwapwa, Husninyo nae kundini
MTM wa kulipwa , kijana namuamini
Pauline sio chapwa, mada zake tathmini
Kaizer si wa kusepwa, hili jeshi la baharini.
Festiledi wa kwanza, nasaha zabubujika
Nyamayao apendeza, akiwepo patashika
wengine sitomaliza, muda umeshatimka
Hawa wakitekeleza, jamii itabadilika.