To KUB Mh. Mbowe

Nadhani kwa hoja yako hii umekurupuka! Majibu ya WK hayawezi kuwa tofauti na yale aliyoyatoa hivi karibuni hivyo kumuuliza tena maswali yale yale ni kutokuwa makini, kupoteza muda na kujidhalilisha.
 
Leo Mbowe alitakiwa awe wa kwanza kuuliza maswali kwa waziri mkuu, na hasa suala la POSHO na MGOMO WA MADAKTARI ila SPIKA kasema Mbowe hayupo , najiuliza amekwenda wapi kama sio hujuma hiii,

Nani kamuhujumu Mbowe apo?
 
Pinda hakuwahi kujibu swali la mh mbowe,mnyika,zitto,lisu,slaa,mnyaa,mara nyingi anaishia kulalamika kulaumu na zaidi kulijibu kisiasa.hamadi amewahi kumuuliza swali akamwambia ndugu yangu hamadi mara nyingi tupo pamoja mbona haukuniambia kama utaniuliza hilo swali?ndipo nilipojua huyu mzee hakuna kitu.vile vile ni mzee muongo.muongo
 
Kiboko yake (PM) wangemuuliza Zanzibar ni nchi au sio nchi? (LoL!)

Lakini hiki kipindi amekiharibu Bi Mkora, kwani baada ya waombaji kuwa wengi, badala ya kufuata principal ya first comes first served kama ilivyo desturi, yeye eti ameamua kuchagua waaliza maswali randomly kadri anavyopenda yeye, hii yote ni njama ya kumuokoa Pinda ndiyo maana aliwahi kupendekeza eti kipindi cha maswali na majibu kifutwe.

Huyu Bi mkora tunashindwa kumuelewa sijui anasimamia muhimili upi wa dola kati ya serikali na Bunge. No wonder leo yeye ndiye amegeuka kuwa mjibu maswali mkuu kuzidi hata PM mwenyewe!
 
serikali ...inashirikiana na.....kufanya mchakato.....ili kushughulikia.......hata hivyo......mapendekezo haya nitayafikisha kwa rais akirudi.....
Bunge lipitishe kanuni ya kupiga marufuku kauli za waziri mkuu serikali na mawaziri wote kwa ujumla kutumia kauli za Mchakato unaendelee,tutalishughulikia n.k.Kwa sababu kauli hizi zinakua kichaka cha kukwepa maswali .Kauli hizi ni kama jipu au bomu ambalo linapolipuka serikali inakua haina majibu.
 
waziri mkuu muongo kuliko wote....

Na leo wakati wa maswali yake, aliulizwa juu ya ucheleweshwaji wa malipo ya pension kwa wastaafu.....alitoa maelezo mengi, ila aliposema kwamba malipo hayo utolewa kila baada ya miezi 6, nikashtuka. Kwa maana nakumbuka mwaka jana aina hiyo mfumo wa malipo waliubadilisha na kuwa kila baada ya miezi 3! Sasa sijui kama serikali iliwapiga changa la macho wastaafu, au Kayanda ndio kama kawaida yake..muongo kuliko shetani!!
 
Ukitizama kwa upande wa pili, hiyo kambi rasmi ya upinzani imena kuwa leo hakuna la muhimu uko bungeni.
Suala la mgomo wa Ma Dr jana na leo limeulizwa lakini kiti cha spika kinasema serikali bado inaandaa taarifa. sasa Pinda si angejibu tu kuwa taarifa itatolewa soon.
Swala la posho hata angeulizwa, wakati ni yeye aliyesema amepewa mamlaka na raisi kulishughulkia na spika akasema limepitishwa. sasa mlitaka aulizwe nini?
PM huwa hajibu maswali, hen it makes no sense kupoteza muda kumuuliza. Hilo l Mabwepand tu aliloulizwa na Mdee hakulijiu ila kaweka siasa tu. Huyu jamaa nadhani anambea baraza livunjwe tu ili apumzike. He is totaly tired
IN SHORT KILE KIPINDI CHA MASWALI KWA PM HAKINA MAANA WALA MANTIKI WALA TIJA. Kinatuongezea bili ya umeme tu kuwasha TV kukiangalia.
 
Suala lenu lipo kwenye mchakato inabidi wananchi waelimishwe ili jambo kwa umakini mkubwa!
 
serikali ...inashirikiana na.....kufanya mchakato.....ili kushughulikia.......hata hivyo......mapendekezo haya nitayafikisha kwa rais akirudi.....
Imagine maneno yote haya hapo bado hajaongea kitu cha maana, sijui siasa itatupeleka wap
 
Eeh unadhani atajibu nini wakati ye mwenyewe hana mda kujua nchi yake inendaje hana lolote alijualo.

Anatoa majibu ambayo yatamfurahisha bosi wake, hata kama hayajibu swali la msingi..Hii ndo Tz zaidi ya uijuavyo
 
serikali ...inashirikiana na.....kufanya mchakato.....ili kushughulikia.......hata hivyo......mapendekezo haya nitayafikisha kwa rais akirudi.....
Imagine maneno yote haya hapo bado hajaongea kitu cha maana, sijui siasa itatupeleka wap
 
Itakuwa ni busara zaidi kama tukivuta subira..ni vitu vinavowezekana kabisa. Anaboa sana huyu ajuza
 
Back
Top Bottom