TMA watabiri mvua kubwa Jumamosi na Jumapili

Watu mna hasira na wanaoishi mab

Sijui waishio mabondeni waliwakosea nini?
Wakati ndo walipakodi wakubwa wanaosababisha zipatikane hela za kupigwa
ili wapigaji wajenge sehemu nzuri.
Hapana siwachukii nawaonea huruma..kwa sbb ni hasara sana kila mwaka unaharibikiwa vitu maji yanaleta uharibifu mkubwa..why ukae mahali pa hivyo? Utasema umejenga nyumba lakini hasara unayopata unaweza jenga chumba kimoja au viwili sehemu salama mnakohamishiwa...
 
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, imetabiri mvua kubwa inyotarajiwa kunyesha tar 27 na 28 Januari 2024. Mvua hizi zimetabiriwa kuwa tarehe 27 Januari 2024 zitanyesha mikoa mitano, Morogoro Kusini, Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe. Aidha kwa siku ya Jumapili Januari 28, 2024 zitanyesha Morogoro Kusini, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Songwe na Iringa.
View attachment 2882451

View attachment 2882452
Shukran sana
 
Usiwadharau,umeshaambiwa wanatabiri ukisubiri inyeshe au wakuthibitishie kama wanavyofanya wenzetu waliojitosheleza kivifaa maji yatakusomba ukiwa umekaa hapo sebuleni kwako.
Sasa we huon hiyo chat inasema Leo akuna mvua je tungepita na huo utabili wao tukajisahau kutia tahadhali Leo si tungepoteza ndugu wengi zaidi ya Hawa mana hapa tulipo asaivi ni vilio vimetanda na tupo juu ya bwana atuna tena makazi
 
Asante kwa Taarifa.

WATU WA MABONDENI CHUKUENI TAHADHARI

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Sijaona Dar es Salaam hapo hivyo ngoja niendelee kurekebisha Kibanda changu hapa Bonde la Mpunga Kinondoni ambacho Kilisombwa na Mvua Kubwa ya Weekend iliyopita.
 
Back
Top Bottom