TMA wananunua rada mpya, hivi ile iliyokula pesa nyingi haifai? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TMA wananunua rada mpya, hivi ile iliyokula pesa nyingi haifai?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuyuku, Jul 26, 2011.

 1. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Waungwana, nakumbuka katika lile sakata la rada tuliambiwa ile rada inafanya kazi za usalama, uwanja wa ndege na mambo ya hali ya hewa. Sasa mbona nakuwa kama sielewi? Someni hapa

  Hussein Issa
  MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA), imenunua rada mpya itakayorahisisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo.
  Kaimu mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Agnes Kijazi alisema ununuzi wa rada hiyo ni moja ya mafanikio yaliyofikiwa na mamlaka katika kuzikabili changamoto za kupima hali ya hewa nchini.

  “Hii ni mojawapo ya mafanikio ambayo Mamlaka imeyapata katika kipindi hiki kifupi ,tutaitumia vyema hii rada ili kuwafahamisha Watanzania kuhusu hali ya hewa kiufasaha zaidi,”alisema.Dk Kijazi alisema mamlaka pia imefanikiwa kupata cheti cha kimataifa cha ubora kinachotambulika kimataifa katika utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa anga.

  “Nilifarajika sana wakati wa kupokea cheti hicho kwa sababu Tanzania ilikuwa ni nchi pekee katika Bara la Afrikakwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara kupata cheti hicho,”alisema.
  Katika hatua nyingine Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu alizindua bodi mpya ya ushauri ya mamlaka hiyo,yenye jukumu la kutoa ushauri kwa Serikali na mamlaka hiyo.

  “Mmepewa jukumu kubwa na mnatambulika serikalini, hivyo mmeaminika naomba ushirikiano wenu ili ikiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto zinazowakabili,’’alisema Nundu.Alisema miongoni mwa changamoto ambazo bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wake Marisson Mlaki ni pamoja na kuboresha CXhuo cha Hali ya Hewa mkoani Kigoma.
   
 2. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Tumekuwa tuaaminishwa hivyo miaka yote.Ukipata fursa ya kutoka nje ya mipaka ya nchi, hii ndipo unapoweza kuelewa hawa jamaa wanasema nini?

  Mbona tunapenda kuwaaminisha wananchi wetu kwamba tumepiga sana hatua kimaendeleo?????!!!! leo utaambiwa ni nchi ya pekee kwenye hili , kesho kwenye lile.... kaah
   
 3. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  kumbe lile rada la awli ni zawadi tulifanye chuma chakavu uone moto wa wamarekani...tuliambiwa dude linauwezo mkubwa sana kutumiwa na nchi kama tz ..ona sasa tumerudishiwa pesa zetu..
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du! Kweli elimu ni kitu muhimu tangu lini rada ya hali ya hewa ikalinganishwa na rada ya Kijeshi... kalagabaho... vioja kuenda mbele.
   
Loading...