TMA toeni utabiri wa mvua za masika

TMA toeni utabiri wa mvua za masika

pacoma

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
650
Reaction score
415
TMA hatuwaelewi kwa mikoa ambayo masika yake inaanza March, Hizi mvua zinazoendelea kunyesha ndio masika imeanza? Tuoteshe mazao au? Mfano Kilimanjaro mvua zinanyesha. Je, za kupanda mbegu au bado ni vuli?
 
145286782_1297174663991514_4904101121982645953_n.jpg
Hali ya hewa kwetu
 
(Kiongozi jaribu kiingia kwenye tovuti ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kuna taarifa zinaweza kukusaidia , hasa doc yenye kichwa cha habari "
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Zamani hatukusubiri vituo mvua ikianza tu tunajua vuli ,masika au za kupandia choroko!
 
HalafuTMA wakitabiri mvua kubwa kesho yake mvua hainyeshi wakinyamaza kimya mvua inanyesha
Huko kwenu hakuna watabiri wa asili? Hawa TMA huwa wanasubiria mvua ianze kunyesha ndio wanaleta wanachoita utabiri sasa sijui huwa wanatabiri nini
 
Zamani hatukusubiri vituo mvua ikianza tu tunajua vuli ,masika au za kupandia choroko!
Maisha yanabadilika au ndio nipo nyuma, mbona hii kitu inajulikana kabisa ni mvua za masika zimeanza baadhi ya mikoa, nimestaajabu mtanzania anasubiri aambiwe ndio aingie shambani, ambacho naona ni jukumu la TMA ni kutoa tamko labda wingi au uchache wa mvua msimu huu, ila kwa kipindi ni masika mkuu au naingia chaka??
 
Kizazi laini laini kuamka pia anatega kengele!

Back
Top Bottom