TMA imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa siku mbili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa siku mbili.

Angalizo hilo limetolewa leo Oktoba 16 na kutaja maeneo yatakayokumbwa na mvua hiyo kuwa ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa kutoka TMA zimesema mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi Oktoba 17,2019 hivyo wakazi wa mikoa tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.

Kwa sababu hiyo athari zitakazotokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Chanzo: Francisdande.blogsport.com
 
Yaani tahadhari inatolewa leo leo na tukio ni the same date.. Hawa wanazidiwa sana hata na viumbe wasioenda shule.. Wenzetu wanaoa tahadhari 7 days before the occurance na wanajiandaa kukabiliana na hali halisi.. hawa wanatoa tahadhari siku hiyo hiyo angali watu wako kujitaftia.. watumie vizuri mitandao ya kisayansi na mitambo waliyo nayo maana ina uwezo mzuri to ila shida ni wenyewe kuinterpret taarifa za hali a hewa.. Ni hayo tu..
 
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa siku mbili.
Angalizo hilo limetolewa leo Oktoba 16 na kutaja maeneo yatakayokumbwa na mvua hiyo kuwa ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa kutoka TMA zimesema mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi Oktoba 17,2019 hivyo wakazi wa mikoa tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Kwa sababu hiyo athari zitakazotokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.
Chanzo: Francisdande.blogsport.com
Kumi na sita ipi tena, leo? Mimi siwaamini kwani nao wanatazama mawingu kama mimi hawana uhakika. Hebu kawaulize walioko baharini nani atawapekekea taarifa hii?
 
Mkuu Miss Zomboko, kila nikionaga uzi wako, huwa nina 'pay attention' vibaya.

Kama ninaendesha huwa sisomi hadi nipaki.

Habari zako huwa zinapakuliwa toka jikoni kabisa!

Yawezekana wewe ni bonge la mwandishi wa habari za kuaminika sema tu haupendi kujiweka wazi.

Ahsante kwa taarifa inayoweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwetu raia.
 
Back
Top Bottom