Hivi haujui kwamba TLS ni chama cha mawakili wa mahakama zetu? Haujui kwamba wao ni watumishi wa mahakama zetu? Haujui kwamba wao huteuliwa na Jaji Mkuu kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa haki mahakamani? Haujui kwamba mwajiri wao ni serikali upande wa muhimili wa mahakama unaoongozwa na Jaji Mkuu ambaye ni mteule wa raisi? Haujui kwamba Jaji mkuu anaweza kumfuta kazi wakili yo yote kwa sababu yo yote na wakati wowote?
And so what Mr
Dr Akili...?
Let us assume, all what you presented in questions are true...
Na wewe ina maana pamoja na udaktari wako hujui kuwa pamoja na kuwa TLS inatoa utetezi wa kisheria kwa wananchi mahakamani, utetezi huo unavuka kuta za mahakama na kuja nje pia..?
Rafiki huhitaji kupaniki wala kuweweseka kiasi cha kujiuliza maswali mengi hivi ambayo ni absolutely irrelevant na kinachokwenda kufanyika tarehe 5/10/2024 J'mosi ktk ukumbi wa Ubungo Plaza - DSM...
Ni kuwa kongamano hili ni sehemu ya majukumu ya TLS kutetea wananchi kisheria na kutoa ushauri kwa serikali nini cha kufanyika kuhusu utatuzi wa ishu fulani ya kisheria (
soma section 4 ya sheria inayounda TLS ujue malengo ya TLS)....
Kumbuka kuwa:
Disappearance, abduction & killings of inncocent civilians hapa nchini ni makosa ya jinai yanayokiuka sheria na haki za watu. Ni jukumu la TLS ku deal na hili ktk scope yao...
Hii haizuii taasisi au vyombo vingine vinavyohusika na haki na uchunguzi kama polisi, mahakama nk nchini kuendelea na kazi na wajibu wao...
Yaani haujui kwamba vyama kama vya madaktari, waalimu na wahandisi ni bora na huru zaidi kuliko hiko chama cha mawakili kwani ajira ya wengi ya wanachama wake siyo na wala hazitegemei muhimili wo wote wa serikali?
Acha udanganyifu na upotoshaji wako...
Kwanza elewa haya:
1. Vyama vyote vya wafanyakazi & kitaaluma viko kwa mujibu wa sheria za Tanzania ikiwemo TLS...
2. As for TLS kuna aina mbili za wanachama mawakili. Wajiriwa wa serikali (public bar) na mawakili wa kutegemea (independent bar)..
3. Though wote hawa (public & independent bar) ni maofisa wa mahakama, tofauti yao ni kuwa wengine direct ni waajiriwa serikalini na hawa wengine wamejiajili wenyewe binafsi. Connection yao na serikali iko kwenye kuwapa vibali (licences) na ulezi kwa kutumia chombo maalumu cha kulinda maadili ya uwakili wao...
4. Kuna utaratibu wa kisheria kumfutia leseni wakili. Jaji mkuu, mahakama au serikali at large haiwezi kuamka tu na kuifuta TLS asubuhi tu kwa tamko eti tu kwa kuwa wanatumia uhuru wao kutoa maoni yao juu ya mambo yanayoihusu nchi yao. Rejea kesi ya Adv. Fatuma Karume na Boniface Mwabukusi....
5. Hiki wanachokifa
Yaani hujui kwamba hso mawakili leo hata kama wakigoma wote nchi nzima hakuna madhara yo yote yatakayotokea isipokuwa wao watakufa kwa njaa?
Wakigoma wote, hata mahakama nazo hazitafanya kazi yake...
Kumbuka wewe mwenyewe umesema hawa ni "waajiriwa wa mahakama". Sasa mfanyakazi akigoma, kuna kazi itaendelea hapo?
Kwa hiyo sio suala la wao kufa njaa tu bali, mambo na mfumo mzima wa utoaji haki utakuwa shaken....
Therefore, it's a two way traffic. Tunategemeana. Tusitunishiane misuli. Our difference & disputes have to resolved amicably kwa kuzungumza na sio ubabe...
Yaani hujui kwamba mafaktari au waalimu au manesi au polisi wakagoma nchi nzima, madhara yake ni disaster na serikali lazima itanyoosha mikono juu?
It's more than disaster kwa mawakili iwapo hawatafanya majukumu yao, yaani kama watagoma...!!
Hivyo kazi ya wanachama wa TLS ni mahakamani tu...
Wrong understanding...!
Kama hujui, unaweza kuuliza Mr
Dr Akili. Acha tabia ya ku - expose ujinga wako wazi kiasi hiki...!
Ukitaka kuelewa vyema majukumu ya TLS kasome
section 4 ya malengo (objectives) ya sheria ya kuundwa/kuanzishwa kwa TLS...
Pamoja na kuwa ni kutetea wananchi wenye kesi mahakamani, pia utetezi huo unavuka kuta za mahakama na kutoka huku nje kama ambavyo wanakwenda kufanya
Hiki anachowaongoza Mwambukusi wafanye nje ya mahakama ni siasa...
Kwa uelewa na ufahamu wako, siasa ni nini kwani..?
In case kama hujui, ni kuwa, siasa ni maisha na maisha yetu ya kila siku ni siasa...
More over, siasa iko kwenye taaluma ya uchumi, iko kwenye taaluma ya sheria, utabibu, elimu, social services etc....
To cut it short, ni kuwa, siasa ndiyo huamua maisha yetu ya kila siku ule nini, ulale wapi, uishije, ulipe kodi kiasi gani, uishi au ufe, upate huduma za afya, elimu, barabara za aina gani nk.....
TLS haijasajiliwa kama chama cha siasa...
Si chama cha siasa lakini inahusika na siasa na vivyo hivyo siasa inaihusu TLS. Au mawakili hawapigi kura kuchagua viongozi akiwe Chura Kiziwi..?
Nakuona wazi kuwa unasumbuliwa na ufahamu mdogo wa mambo haya. Hili ndilo tatizo lako...
Ondoa mashaka na wasiwasi kwani kinachokwenda kufanyika ktk kongamano la tarehe 5/10/2024 J'mosi Ubungo Plaza - DSM ni siasa isiyofanywa na chama cha siasa bali ni mjadala kuhusu athari za maamuzi ya kisiasa na wanasiasa ktk maisha ya watu ktk mtazamo wa kisheria. Umeelewa hapo..?
Hii ni haki na wajibu wa kila raia ukiwemo wewe
Dr Akili
Serikali kupitia mhimili wake wa mahakama inaweza na inapaswa kumfuta kazi ya uwakili wa mahakama mara moja huyu Mwambukusi, akatafute kazi nyingine...
Haina shaka...
Kama wana sababu za msingi, waanzishe huo mchakato tuone mwisho wake....
Kama iliweza kumfuta Fatma Karume, mjukuu wa Baba wa Taifa la Zanzibar, sembuse Mwambukusi? Mwache aendelee atakipata anachokitafuta.
Naona na wewe ni miongoni wa "wasiojulikana" maana unaweweseka kwelikweli na kurusha ngumi hewani hovyo....
4Rs za Mama zisiwe kisingizio. Uvumilivu aka resiliency una mwisho wake.
Haya 4Rs ulikuwa ni utapeli wa kisiasa na kama wimbo huu bado upo, basi unaendelea kuwa utapeli huohuo...