Kuna viumbe wameanza kucheza na kazi za uwakili, juzi jamaa kanunua eneo na katika mauziano akamwagiza dalali amtafute Wakili na huyo dalali akamleta MTU aliyejitambulisha kuwa wakili na wakakamilisha biashara.
Baadaye tukiwa kijiweni tukasikia jamaa mmoja analalamika kuwa ametapeliwa kwa kuthibitishiwa baadhi ya nyaraka zake kuwa ni halisi kumbe muhuri uliotumika siyo wa Wakili aliyesajiliwa bali ni matapeli wamechonga muhuri.
Huyo jamaa aliyekuwa analalamika akadai jina la muhuri uliotumika amebaini alipo kwenye majina ya mawakili waliosajiliwa nchini.
Tukashtuka na kuchukua jina la yule Wakili aliyegonga mkataba wa mauziano ya Kiwanja cha rafiki yangu nakuangalia kwenye majina ya mawakili waliosajiliwa nchini nako tukakuta jina ilo halipo..tulipomfuatilia yule dalalali atusaidie kumpata yule wakili ,Dalali akatuambia hana mawasiliano naye kwa sababu walikutana naye kijiweni eneo la Buzuruga hapa Mwanza,
Hadi sasa tunamtafuta huyu mtu atujampata. Hii ni Mwanza,je Arusha na Dar hali ipoje?
Wito wangu ni kwa mawakili wote nchini kulinda mihuri yao lakini pia watanzania waelimishwe umuhimu wa kupata mawakili wenye kuaminika kwani mikataba inagharimu fedha nyingi wanazolipwa mawakili na pia inapotokea mgongano baina ya pande mbili Wakili husika anatarajiwa kumsaidia mteja wake kupata haki.Hasa utapataje haki endapo wakili aliyekusaidia kutengeneza mkataba au nyaraka flani atambuliki na chama cha mawakili?
Nasikia wapo pia wanafunzi katika kuomba mikopo na nafasi za vyuo wameingia kwenye mikono ya matapeli hawa na taarifa zisizo rasmi zinadai mawakili feki wapo sana maeneo ya mahakama za chini nchini lakini wapo pia wanaodiriki kuchonga mihuri ya mahakama na kuitumia kucetify hati mbali mbali pamoja na kutengeneza viapo vikiwemo vya kuzaliwa.
Hivyo tutambue kuwa kuna aina hii mpya ya uhalifu ambayo inanajisi taaluma za watu lakini pia inaweza kuisababishia hasara Jamuhuri na watanzania kwa jumla.
Naandika nikiwa na uchungu kwani ndugu yangu amepoteza milioni Tatu na nusu kumpa wakili feki ambaye naamini hana taaluma yoyote ya sheria.
TLS na vyombo vya dola tuondoleeni hawa viumbe wanaotutia umaskini kwa kututengenezea hati na matamko feki.......
Mwana JF, tumia Uzi huu kutaja baadhi ya maeneo walipo maharamia hawa wa taaluma huku ukitoa yako ya moyoni kama limewahi kukukuta....