TLS chini ya Lissu kama kweli wanaitakia mema Tanzania waungane kuzima wizi wa Acacia

HEKIMA KWANZA

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
2,942
3,937
Tumesikia mengi kuhusu Acacia kutuibia Watanzania kwa kutumia mikataba, tena iliyoandaliwa na Watazania wenzetu. Kama taifa, hatuwezi kuendelea kulalamika na kunyoosheana vidole, ni lazima tuchukue hatua. Sheria sio Misahafu. Sheria zimewekwa na binadamu na zinaweza kufutwa au kurekebishwa na binadamu pia.

Pamoja na nguvu ya kifedha waliyonayo Acacia Watanzania wakiungana tutashinda hii vita ya kiuchumi. Sasa, TLS kama kweli wanaitakia mema Tanzania waungane na kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta vifungu vya kinyonyaji na kuhakikisha kila kinachovunwa kwenye ardhi ya Tanzania kinalipiwa kwa haki, na sio kutumia huu ujanja wa 'commercially viable'.

Ni wazo.
 
Lissu ashalazwa kisutu na mkapa plus serikali ya magufuli kwa kutetea hayo madini yasiuzwe kinyemela! Leo hii ndio mnakurupuka mnataka awasaidie MTU mliemtesa? Hata ningekuwa mm bora niside na upande wa pili ili tuwakalishe mahakamani nanyie msome namba uzalendo uzalendo pyuuuuu ndio mnajua Leo nyie mafirauni
 
TLS will 100% support if and only if the legal ways are followed, kupitia mitini kwa kamati za maprofesa wa vitabuni na si wataalam on the ground si sawa. 10 min tu boss karudi na mrejesho wa ripoti nzima, met be an alien can do.
Weka tume huru ya uchunguzi kukiwa na wawakilishi wa kimataifa au TZ iwashtaki ACACIA on the course of which uchunguzi utafanyika kujua mbichi na mbivu.
 
*MAJIBU YA LISSU KWA MAKADA WA CCM*

Khamnemba.

Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
 
TLS will 100% support if and only if the legal ways are followed, kupitia mitini kwa kamati za maprofesa wa vitabuni na si wataalam on the ground si sawa. 10 min tu boss karudi na mrejesho wa ripoti nzima, met be an alien can do.
Weka tume huru ya uchunguzi kukiwa na wawakilishi wa kimataifa au TZ iwashtaki ACACIA on the course of which uchunguzi utafanyika kujua mbichi na mbivu.
Maprofesa waandika majibu ya kisiasa badala ya kisheria na kimikataba nani atawathamini?
 
Tumesikia mengi kuhusu Acacia kutuibia Watanzania kwa kutumia mikataba, tena iliyoandaliwa na Watazania wenzetu. Kama taifa, hatuwezi kuendelea kulalamika na kunyoosheana vidole, ni lazima tuchukue hatua. Sheria sio Misahafu. Sheria zimewekwa na binadamu na zinaweza kufutwa au kurekebishwa na binadamu pia.

Pamoja na nguvu ya kifedha waliyonayo Acacia Watanzania wakiungana tutashinda hii vita ya kiuchumi. Sasa, TLS kama kweli wanaitakia mema Tanzania waungane na kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta vifungu vya kinyonyaji na kuhakikisha kila kinachovunwa kwenye ardhi ya Tanzania kinalipiwa kwa haki, na sio kutumia huu ujanja wa 'commercially viable'.

Ni wazo.
TLS ipi? Hii iliyotaka kufutwa? Na Tundu huyu huyu aliyefanyiwa figisu asichaguliwe?

Kwani mikataba ali sign nani na hao ACACIA? TLS?
Jamani basi tufukirie kidogo.
 
Lissu ashalazwa kisutu na mkapa plus serikali ya magufuli kwa kutetea hayo madini yasiuzwe kinyemela! Leo hii ndio mnakurupuka mnataka awasaidie MTU mliemtesa? Hata ningekuwa mm bora niside na upande wa pili ili tuwakalishe mahakamani nanyie msome namba uzalendo uzalendo pyuuuuu ndio mnajua Leo nyie mafirauni

Mkuu:
Punguza munkari, nyumbani ni nyumbani tu. Ngombe akiumia mguu hurudi zizini.
Mh. Lissu asikatishwe tamaa na hao wachumia tumbo.
Wataumbuka wote mmoja baada ya mwingine, huko ndio kuiva kwa maharage ni lazima yachemke na kupinduka pinduka. Muda ndio mwalimu.
 
TLS tena? Yaani madudu mfanye nyinyi tena kwa dharau na kebehi kule kitalani halafu Leo eti tuungane... Mwambieni Mwanasheria Mkuu Wa serikali awasaidie, PIA Mtemi Chenge, Werema, Tulia Akson na Mwakyembe wanaiweza hii kazi, vizuri Sana, kutoka kwetu sisi tegemeeni Tu maombi na dua, mengine fanyeni wenyewe kama mnavyofanyaga kwenye majanga mengine ya kitaifa. Pumbavu kabisa.
 
Aombwe kwanza msamaha!
Yaaani eti ajipeleke kuanza kupambana bila kualikwa!

Mpelekeni kabudi
 
Hao mnaowageukia na kuwaita wezi leo hawakujipa wenyewe hiyo migodi,ni washirika wenu katika kuliibia Taifa.Mikataba hiyo inayowaruhusu watuibie inatunzwa kwa "makabati ya chuma" pale magogoni huku ikiwa imegongwa mihuri ya "SIRI" ili tusiweze kuihoji.

Acheni kulia machozi huku mkiwa mmepiga mbizi baharini,wawekezaji hao mnaowaita wezi,mikataba yao ilijadiliwa na baraza la mawaziri chini ya usimamizi wa Rais wa JMT,kana kwamba haitoshi,karamagi alisafiri hadi Hotelini Rondon kwa kutumia kodi zetu ili aende kukamilisha dili la kuliibia Taifa lililofanywa kati ya Baraza la Mawaziri na washirika wenu katika wizi.

Serikali inayojaribu kuuhadaa umma kwa kupiga kelele za kinafiki,ndiyo hiyo hiyo iliyoketi na kupitisha mikataba ya kilaghai inayozidi ile ya Kina Sultani Mangungo wa Msevero.Mwambieni anayepiga kelele na genge lake la maccm walikula njama za kumfukuza Mh.Zitto bungeni eti kwa sababu alikuwa amesimama kidete kuzuia upolaji huu kupitia Buzwagi.

Wakati bunge linamfukuza Zitto,Magufuli alikuwa bungeni,mbona hakutoka bungeni kama ishara ya kupinga kutimuliwa kwa Zitto ambako kulitokana na yeye kuonekana anatishia kuitia mchanga keki ya kifisadi iliyosainiwa na Serikali akiwemo Magufuli?

Kelele zenu ni za kinafiki na wote wanaoshangilia "sarakasi hizi" ni wanafiki wa kiwango cha lami.Endeleeni kuvumilia na muwaache wazungu warudishe kile walichowahonga ili ninyi muwakabidhi hiyo migodi.
 
TLS tena? Yaani madudu mfanye nyinyi tena kwa dharau na kebehi kule kitalani halafu Leo eti tuungane... Mwambieni Mwanasheria Mkuu Wa serikali awasaidie, PIA Mtemi Chenge, Werema, Tulia Akson na Mwakyembe wanaiweza hii kazi, vizuri Sana, kutoka kwetu sisi tegemeeni Tu maombi na dua, mengine fanyeni wenyewe kama mnavyofanyaga kwenye majanga mengine ya kitaifa. Pumbavu kabisa.

Sumaye aliyemuweka ndani Lissu si wako pamoja?
 
Tumesikia mengi kuhusu Acacia kutuibia Watanzania kwa kutumia mikataba, tena iliyoandaliwa na Watazania wenzetu. Kama taifa, hatuwezi kuendelea kulalamika na kunyoosheana vidole, ni lazima tuchukue hatua. Sheria sio Misahafu. Sheria zimewekwa na binadamu na zinaweza kufutwa au kurekebishwa na binadamu pia.

Pamoja na nguvu ya kifedha waliyonayo Acacia Watanzania wakiungana tutashinda hii vita ya kiuchumi. Sasa, TLS kama kweli wanaitakia mema Tanzania waungane na kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta vifungu vya kinyonyaji na kuhakikisha kila kinachovunwa kwenye ardhi ya Tanzania kinalipiwa kwa haki, na sio kutumia huu ujanja wa 'commercially viable'.

Ni wazo.
1998,wakati bunge la kina JPM,Chenge,Mkapa na JK wakipitisha sheria za madini kwa hati ya dharura,Tundu Lissu alikuwa "korokoroni" kwa kuipinga miswaada hiyo,CCM walipitisha mikataba hii kwa uwingi wao na kura za "NDIOOOOOOO"
 
nashauri tls iwafikishe mahakamani mkapa,jk na wabunge wa ccm wanaoituikia ndiooooooo...wakishasaidia hawa kufungwa waende kwa acacia kwa ajili ya kubadilisha mikataba..fair and square
 
Back
Top Bottom