Elections 2010 TLP yapata mgombea urais mpya

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Siasa, Tanzania Labour Party[ TLP] juzi kilifanikiwa kumpitisha Mutamwega Mugahywa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Mkutano huo uliowakutanisha wananchama wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam na jumla ya wanachama wawili walikuwa wakigombania nafasi hiyo.
Katika kinyang’anyiro hicho alikuwa akigombania Muamwega Mugahywa na Maxmilian Lyimo ambapo, Mugahywa aliibuka kidedea na kupata kura 73 sawa na asilimia 91.76 na Lyimo kuambulia kura 11 sawa na asilimi 9.24 kati ya kura 84 zilizopigwa.
Mara baada ya uchaguzi huo kumalizika mgombea huyo aliwashukuru wapiga kura kwa kumchagua na kupa heshima hiyo na kuahidi kupeperusha bendera ya chama hicho vyema bila kuwangusha wanachama na kulta mapinduzi ndani ya chama hicho.
Alisema anatarajia kufanya kampeni zake kwa kutumia helikopta atakapokuwa akitembelea wapiga kura wake mikoani na anatarajia kuwa rais wa nchi hii na akiwa madarakani anatarajia kuchagua waziri mkuu mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii
 
MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Siasa, Tanzania Labour Party[ TLP] jana kilifanikiwa kumpitisha Mutamwega Mugahywa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika kinyang’anyiro hicho alikuwa akigombania Muamwega Mugahywa na Maxmilian Lyimo ambapo, Mugahywa aliibuka kidedea na kupata kura 73 sawa na asilimia 91.76 na Lyimo kuambulia kura 11 sawa na asilimi 9.24 kati ya kura 84 zilizopigwa.
 
mwenyekiti anamsifia mgombea wa chama kingine sasa mgombea wake sijui atamsaport nani
 
mwenyekiti anamsifia mgombea wa chama kingine sasa mgombea wake sijui atamsaport nani

Mrema ameshatangaza kumpigia debe Kikwete, huyu mgombea wa TLP atakuwa yatima. Hata siku anachaguliwa Mrema alirudia support yake kwa Kikwete, alisema wazi kuwa hakuna zaidi ya Kikwete. Akaongeza kitisho kama wataendelea kumshtumu kwa kumkubali JK basi atahamia CCM. Bora TLP wangemwambia aende zake CCM tu.
 
Atakuwa anatumia ilani ipi ya uchaguzi ya CCM au ya TLP.


Heshima kwako Luteni,

Hivi watanzania wanachagua chama kwasababu ya ilani ??????.Mkuu hakuna cha ilani wa la nini ingekuwa ilani inafuatwa leo hii Tanzania ingekuwa na mahakama ya Kazi ohoo sorry mahakama ya Kadhi.Uchaguzi wa Tanzania umebase zaidi kwenye matumizi ya fedha na wizi wa kura.Ikiwa chama kimejiandaa vizuri kwa maana ya kuiba kura,kuonga wapiga kura,kutumia vyombo vya dola na mambo mengine mengi ya hovyo ni lazima kitashinda.
 
Mwenyekiti wa TLP Mheshimiwa sana Mrema amenukuliwa akiipigia debe la nguvu CCM na kudai kuwa Jakaya Kikwete hana mpinzani! Kwa nini sasa TLP ijisumbue kuweka mgombea Uraisi wakati wao wenyewe wameishampitisha Kikwete kuwa hana Mpinzani???:mad:
 
Mrema hajui asemalo, Anasema yeye hagombei sababu anataka kuongeza nguvu bungeni ukweli ni kwamba kesha pima na kuona urais atafanya kuusikia tuu kwenye vyombo vya habari. Kwanini amdanganye mwenzake akagombee uraisi wakati yeye mwenyewe anampigia debe Kikwete? angemshauri na mgombea uraisi wake agombee ubunge kama kweli anataka kuongeza nguvu za wapinzani bungeni. Mrema asitudanganye tuchanganye akili zake na zetu yeye tunamjua ni kada na muumini mzuri wa chama cha Kijani.
 
njaa mbaya yaani kina mrema wameshaona urais watausikia kwenye bomba tu wanajaribu bahati yao kwenye ubunge, sasa cjui mzee wa kiraracha anataka kwenda kwao marangu au? nadhan wau hawajaelewa dhana ya upinzani, suala si kushindwa ni kudumisha upinzani ili serikali ifanye kazi zaidi na hapo ndio tunajua huu mfumo wa vyama vingi ni wa nchi tajiri kwani kwa bongo ukikosa ubunge au urais ndio umekwisha! sasa ulaya hata mkosa urais ni tajiri so njaa hana
 
Huyo dogo Mutwamwega Mugayhwa sijui ameingia vipi katika mtego wa Mrema; the guy was very intellegent and serious kiasi kwamba nashangaa kuwa bado yuko TLP na Mrema! Nina wasiwasi kuwa pengine nayeye ameshajiunga kwenye kambi ya Mrema Vs Upinzani; kama angejiunga na Chama makini cha upinzani huenda angewapa taabu sana CCM katika Ubunge lakini inawezekana ameshapoteza matumaini ama anapigana vita dhidi ya Upinzani.
 
WANATAFUTA KAZI YENYE MASLAHI MAKUBWA. TENA WAPENDA SANA UBWANA.
WAITWE WAHESHIMIWA ILA HESHIMA HAWANA.
WASIFANYE KAZI BALI WAPATE WA KWANZA. TENA SIO WAOGA KUIMBA WIMBO WA UMASIKINI.
JAMANI WAZEE HAWA WANATUMALIZA. HEBU TUWAULIZE WANAPELEKA WAPI PESA WANAZO MIMINIWA? AU WAMEKUA KAMA WALEVI? WANAIBIWA NA WAZUNGU WAKILEWA HAYO MAJIGAMBO. :"TUWAOMBE WAFANYE UZALENDO WAACHE UMIMI TUIMBE SISI SOTE NI NDUGU. TENA ISIWE MWENYE KASHIKA NI CHAKE ILA NI CHETU. NIA YANGU NI KUONA NA KUSIKIA MNANIUNGA MKONO KWA HILI\.....! WAPEWE WALE WAPYA, NAJUA PIA HAWAWEZI, BALI NAO WAONJE KEKI YA TAIFA (MSHAHARA WA SIASA INALIPA) ...... MAANA HAKUNA WA KUMFIKIRIA MWENZAKE MIMI KWANZA!! Nipeni kula jamani,. mkinichagua nitanunua kiwanja, nitanunua gari nitalewa pombe, nitaenda disko sana, na wapambe wangu nitawa panga mbele. HAPO JE,WEWE HAZITA KUFIKIA SENT KIDOGO? Kama bado wewe nitakupa kazi ya kusimamia ujenzi wangu awamu ijayooooh. ila kwa sasa pole sana!
 
Ni vema TLP wakampa Mrema kadi nyekundi ili arudi CCM kwa kufukuzwa chamani ili akose nguvu
 
Back
Top Bottom