TLP waungana na CUF kudai serikali tatu CDM wanasemaje?

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Katibu Mkuu wa TLP Hamad Tao jana alisema chama hicho kinataka katiba iruhusu serikali tatu madai ambayo tumeyasikia toka kwa chama cha wananchi CUF, je kauli ya Chadema chama kikuu cha upinzani kuhusu serikali tatu ikoje kwanini wanaogopa kuwa wazi kwa hilo au wanasubiri kuona upepo unakoelekea? wanatakiwa wawe jasiri kuongoza mapambano siyo kuogopa.
 
CDM bado hawajui wanachotaka. Bado wako bize na mikakati ya kumuondoa zito kabwe kwenye chama chao kwanza. wakishamaliza hilo ndiyo wataanza kufikiria wanataka nini.
 
Swala la KATIBA sio la CDM ni la wananchi wa Tanzania. wewe kama mtanzania unasemaje?
 
Chadema msimamo wao ni serikali tatu hilo lilikuwepo kwenye ilani yao ya uchaguzi ya mwaka huu,Wachangiaji wote hapo juu naona hamjui lolote huhusu mambo yaliyokuwepo kwenye ilani ya Chadema.hao TLP wamedandia gari la chadema kama CUF walivyodandia gari la katiba la Chadema.
 
Kauli ya CHADEMA uliomba kali hili sio; tukutane Bungeni Dodoma ndiko jibu lako litakalopatikana.
 
Chadema msimamo wao ni serikali tatu hilo lilikuwepo kwenye ilani yao ya uchaguzi ya mwaka huu,Wachangiaji wote hapo juu naona hamjui lolote huhusu mambo yaliyokuwepo kwenye ilani ya Chadema.hao TLP wamedandia gari la chadema kama CUF walivyodandia gari la katiba la Chadema.

Ubarikiwe mkuu kwa kuwaeleza msimamo wa CDM juu ya muundo wa muungano,kwani wote waliochangia awali waliamua kuupotosha umma juu ya suala hili.Ama kweli sasa naungana na waliosema bila utafiti,hakuna kuzungumza!
 
Chadema msimamo wao ni serikali tatu hilo lilikuwepo kwenye ilani yao ya uchaguzi ya mwaka huu,Wachangiaji wote hapo juu naona hamjui lolote huhusu mambo yaliyokuwepo kwenye ilani ya Chadema.hao TLP wamedandia gari la chadema kama CUF walivyodandia gari la katiba la Chadema.
Unaongea usiyoyajua, au wewe umeanza kuisikia CUF baada ya upepo wa CDM kuvumia kwenu? kwa taarifa yako sera ya serikali tatu CUF wameanza kuiweka tangu uchaguzi wa kwanza kabisa wa 1995. Usikurupuke ndugu.
 
Katibu Mkuu wa TLP Hamad Tao jana alisema chama hicho kinataka katiba iruhusu serikali tatu madai ambayo tumeyasikia toka kwa chama cha wananchi CUF, je kauli ya Chadema chama kikuu cha upinzani kuhusu serikali tatu ikoje kwanini wanaogopa kuwa wazi kwa hilo au wanasubiri kuona upepo unakoelekea? wanatakiwa wawe jasiri kuongoza mapambano siyo kuogopa.
Kwani tlp sio watanzania? wao wana haki zote kama raia wa nchi hii kusema wanavyoona. Chadema tuna haki ile ile kwa hiyo la ajabu hata uweke thread hivi ni nini kama si umbeya tu na ushambenga unakusumbua? Kudadadeki wee.
 
Back
Top Bottom