Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Mgombea wa Urais Kupitia chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Yustas Rwamugira amesema kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha Maiti hazizikwi na serikali kutokana na ndugu kushindwa kulipia Pesa za mochwari hivyo atahakikisha anafuta malipo ya kuhifadhi maiti katika Hospitali za serikali. Akizungumza baada ya kuchukua fomu ya kugombea katika ofisi za tume huru ya Taifa ya uchaguzi Rwamugira amesema kuwa atahakikisha matibabu yanakuwa bure kwa watanzania wote.