Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Taasisi ya Taifa Letu, Kesho Yetu (TK) Movement Mkoa Kagera imesema haitakubaliana wala haitamsikiliza mtu yeyote mwenye kuja na kauli za kuwapotosha wananchi kuwa wasishiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2025
Hayo yamejiri katika Kikao cha Wilaya Bukoba DC kilichowakutanisha Viongozi wa taasisi hiyo pamoja na Viongozi wa Kata zote
Akizungumza Mratibu wa Mkoa Kagera Ndg Charlisious Charles aliwataka Viongozi hao kuwa wasikubali kudanganyika kwa maneno yanayotolewa na baadhi ya watu kuwa watanzania wasishiriki Uchaguzi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Ndugu Viongozi wenzangu, kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitoa kauli za kuhamasisha watanzania kutoshiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Kwa niaba ya Kamati ya Uratibu Mkoa Kagera ninaomba kuwaambieni kuwa tuwapuuzeni watu hao kwani hawana nia njema na Amani ya Taifa letu” Amesema Charles .
“Uhuru wa Taifa letu umepiganiwa na watu walitoka jasho na damu, hivyo tusikubali watu wachache watudanganye na kuivuruga amani ya Nchi yetu. Uchaguzi ni takwa la kikatiba ambalo haliwezi kuvunjwa na mtu kwasababu ya sababu zake mwenyewe” Charles amesema.