Kazi ya kutembelea mitandao ya jamii kama vile facebook, Insta ili kuangalia nani kamsema mtawala vibaya ili wamminye ndiyo kazi ya mashirika ya kijasusi yaliyo muflisi, yanaacha mambo makubwa kama vile Thamani ya kura ya mwananchi, Uhuru wa watu, Demokrasia, Utawala bora, Kulinda rasilimali za nchi, Supremacy ya Katiba, Umakini katika kutunga sheria za nchi, Kupitia mikataba mikubwa kabla ya kusainiwa na kutoa recommendations muafaka, Kufanya Vetting ya maana kabla ya kuwakabidhi watu mamlaka makubwa, Kuspearhead Diplomasia yenye mrengo wa Uchumi, Kuhakikisha Teuzi zinareflect umoja wa kitaifa badala ya muonekano wa udini , ukabila au ukanda, Kuhakikisha kizazi kijacho kinaandaliwa mapema kupokea kijiti cha maendeleo na uongozi wa Taifa, Kusponsor tafiti kupitia taasisi zilizochini ya mwavuli wake ili kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa, Kuwalinda watu wote ambao ni potential leaders hata kama ni wa kutoka chama cha upinzani wasidhuriwe maana watu hao muda wowote wananchi wanaweza kuwakabidhi dhamana. Hizo ni baadhi ya kazi adhimu za Mashirika ya Kijasusi duniani siyo kutorture watu au kuwaharibia watu future kwa sababu wanatoa comments dhidi ya mtawala!. Mtawala ni sehemu muhimu ya Taifa lakini siyo Taifa lenyewe, na shirika la Kijasusi lazima liwe ni kwa ajili ya Taifa siyo mtu au chama fulani cha siasa!