Unaogopa nini kutaja jina la hiyo benki?
Nikweli kuna mambo yanazingua sana kwenye mfumo wetu wa kibenki mojawapo ni hili la TISS. Sijui kwann wana cutt-off time na jambo lenyewe ni online. Lkn kwenye swala la mwisho alhamis rudi kwenye hiyo benki ongea na mwingine yawezekana huyo mtu hajui, maana kuna benki nyingine nilishafanya weekend na mzigo ukaenda, pia muda wa saa sita pia sidhan km ni sahihi.
Jambo jingine ni hitaji la kutaka mtu unayemuwekea cheque asaini slip na cheque pia!! nmb walinikatalia mpaka jamaa asign na huku namlipa mtu yupo more than 450km away!! nikamuuliza je ingekua cash akasema hiyo haina shida, nikauliza je ingekua nalipa ada ya shule? akanyamaza nikasepa 😡😡
HahahaKidogo nihusianishe na MASOFA
Jr[emoji769]
bbc , Kwa nini TISS iwe hewani saa za kazi tu? Kwa nini isiwe hewani mida yote? inawezekana isiyofanya kazi 24/7 ni hiyo TACH. Lakini wenye mabenki husema ni TISS ya kibenki mwisho Alhamis mchana.Mlenge, hao waliokueleza hivyo huenda ni wavivu tu wa kazi. TISS ipo mda wote wa saa za kazi, ni mfumo wa malipo unaohusika na kuhamisha pesa kutoka akaunti moja kwenda nyingine (funds transfer). Kwa sasa hivi kwa jinsi mifumo ilivyoboreshwa unaweza kuhamisha hela ndani ya nusu saa zikawa zimefika kwenye akaunti husika. Hundi (cheques) zina mfumo wake uitwao TACH (Tanzania Automated Clearing House). Kidogo nikijuacho ni hicho.
Nijuavyo mimi, "cut-off time" ya TISS ni saa 4 usiku kuanzia J3 mpaka J'mosi na mchana kwa siku ya J2. Huu ni mda ambao karibu taasisi zote (Benki kuu, benki za biashara na Serikali) zinakuwa zimemaliza kazi ya siku. Kumbuka hizo "transfers" zinafanywa na wafanyakazi.bbc , Kwa nini TISS iwe hewani saa za kazi tu? Kwa nini isiwe hewani mida yote? inawezekana isiyofanya kazi 24/7 ni hiyo TACH. Lakini wenye mabenki husema ni TISS ya kibenki mwisho Alhamis mchana.