Acheni siasa,njaa ipo Tanzania,wala sio tishio la njaa.Hivi unapata faida gani kudanganya?Njaa Iko wapi Tanzania. Acha uongo. Kukiwa na janga la njaa, hata ukiwa na hela hutapata chakula kutoka eneo lenye baa la njaa. Nani ana hela amekosa chakula (viazi, mchele, maharage, mtama, mihogo, maboga) nchi hii. Utasema vijijini, kwani kama wana hela si waende mjini wakanunue kuna kila kitu kipo. Tatizo ninalolikubali ni kwamba uwezo wa kununua kwa kiingereza purchasing power ndio shida ya walio wengi kwa sasa. watoto wao waliokuwa wanamwaga mahela hadi vijijini wameminywa hawana namna. Swala la upngufu wa chakula kwa baadhi ya maeneo ni jambo la kawaida Tanzania na serikali zimekuwa zikichukua hatua. Karagwe walipelekewa mahindi vyombo vya habari vilituhabarisha, Chemba kulipogundulika wanakula mahindi yenye sumukuvu, serikali iliwapelekea mahindi mbadala. Msikuze mambo kutisha watu. Mmeishiwa hoja, mmeshikilia hoja ya njaa. Serikali iko kazini. Raisi sio mjinga, hawezi kutangaza nitapeleka chakula kila mahali, mbona na walionachi watauza au kuficha ili kudai hawana wapewe. Acheni siasa