Mworombo01
Senior Member
- Nov 9, 2016
- 113
- 82
Nishatumia hiyo mkuu naishia kukutana nao tu. Kama ukizima taa dakika mbili tu ukaweka mfano kitambaa cheupe kwenye kochi ukijawasha utadhani maua..dooo! Hatare tu.Unaogopa mende mkuu? Ishi nao vizuri tu kwa nini muuane??[emoji16][emoji16](nakutania) kuna dawa fulani hivi iko kwenye vipakt vya kijani ila yenyewe ni ya ungaunga hivi inaweza kukusaidia. Ulisha wahi kuitumia nayo?
Sawa Mkuu nitashukuru sanaKuna dawa hivi mende wanakufa wote, nikiwa nyumbani nitapiga picha nikuwekee hapa. NIQUOTE ILI NIKUMBUKE.
Utadhani ninmradi wa watu aiseeNjaaa iyo itakuwa wametumwa
Habari wadau!
Tafadhali mwenye kujua dawa au suluhisho la mdudu mende tafadhali naomba anisaidie maana kila kukicha mende ndani wanaingezeka licha ya kupiga dawa kila mara ukiwa na moyo mdogo unaweza hisi wametumwa. Viko vijimende vidogovidogo na mibaba yao yaani ndani hakina amani tena.
Nimegundua siko peke yangu wengi tunapata shida hiyo.
Tafadhali msaada.
Nilijua kwangu tu daa kumbe wengi , itakuwa wanatoka nje ngoja tusubili
Kama ni hivyo itakua kina Chong Lee...Nilijua kwangu tu daa kumbe wengi , itakuwa wanatoka nje ngoja tusubili
Shukrani mkuu. Nitaitafuta.Poleni sana ndugu zangu kwa matatizo ya mdudu mende na ndugu zake. Kuna dawa inaitwa FIPROFARM. Nawahakikishia, ukipiga hiyo ndani na nje ya nyumba yako. Hakuna mende atayethubutu kuja kuongea nawe tena hapo nyumbani. Dawa hiyo ikauzwa kwenye Maduka ya dawa za mifugo na kilimo.
Ila nasikia ni mradi kweli huo. Kuna jamaa alitoa uzi wake humu kuhusu kufuga mende.Utadhani ninmradi wa watu aisee
Sawa mdau, hiyo dawa inaitwaje unayoochea makaro? Hilo la vyombo baada ya kugundua wanapigaga disco usiku nikapiga marufuku kulaza vyombo vichafu.Jitahidi ndani uiweke vyombo vichafu ikiwezekana usiku kabla ya kulala Dada aoshe vyombo.... Mende wakikosa mabaki ya chakula wanaama wenyewe.... Alafu ukiweza nenda kariakoo kama unaishi dar nunua dawa ya kuuwa mende mara nyingi ndiyo inayotumika kuoshea mbwa au ng'ombe, mimi uwa ninachukua kichupa kimoja Nina mix na maji ndoo ya liter 20 Nina imwaga kwenye makaro madogo linalotoka jikon, choon na bafuni Mida ya usiku ninapoenda kulala.. Asubuhi ninakutana na maiti za mende kama Mia juuu ya makaro...
Naisubiri piaKuna dawa hivi mende wanakufa wote, nikiwa nyumbani nitapiga picha nikuwekee hapa. NIQUOTE ILI NIKUMBUKE.
pangilia mazingira yako vizuri... epuka kuacha vyombo bye bye masalia ya chakula bila kuvisafisha pia hakikisha kuna mwanga wa kutosha ndani kumbuka mende wanaogopa sana mwanga /photophobia.Habari wadau!
Tafadhali mwenye kujua dawa au suluhisho la mdudu mende tafadhali naomba anisaidie maana kila kukicha mende ndani wanaongezeka licha ya kupiga dawa kila mara ukiwa na moyo mdogo unaweza hisi wametumwa. Viko vijimende vidogovidogo na mibaba yao yaani ndani hakuna amani tena.
Nimegundua siko peke yangu wengi tunapata shida hiyo.
Tafadhali msaada.
Mkuu hiyo nimepuliza sana na nyingine za kinyunyiza lakini ndo kwanza wanazaliana.Puliza HIT ni dawa ya mbu. Inaua Kila kitu. Puliza Sasa kila sehemu uvunguni kwenye Kochi, kabati n.k baada ya nusu saa lete marejesho.