white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,618
- 13,896
Hawa AGAPE,ambao wana king'amuzi chao cha ting,wamebadilisha mfumo wa urushaji matangazo toka dvbs kwenda dvb t2,hivyo wakawataarifu wateja wao kuwa wanatakiwa kuzirudisha zile decoder ambazo kwa mfumo wa sasa hazifanyi kazi,na wanapiga simu,kuwa nenda na remote na decoder ili upate mpya ambayo ni HD,Cha ajabu ukifika pale wanapokea na kukupa form ujaze na ulipe tsh.60,000,ambayo ni monthly subscription ya miezi 6,ijayo!!eti hadi january mwakani!ni kama huna pesa hiyo basi hawakupi decoder hiyo mpya!sasa hapa inakuwaje kubadilisha decoder kuhusishwe tena na kulipia tena miezi 6,angalau ingekuwa mwezi moja!mtu decoder ile ya awali aliinunua hivyo ni mali yake,inakuwaje kwenye kubadilisha umwambie ni bure ila unatakiwa ulipie malipo ya miezi 6 mbele!je kama yeye anataka zile 5 tu za kitaifa ambazo hatakiwi kulipia?na ni taasisi ya dini hii,kweli watanzania tuna maadui wengi ukigeuka huku unakula ya kichwa,kule unakula ya shingo!