Sangara, tunajadili sana swala hili kwa kuwa linahusisha raia wa nchi nyingine, foreigners wanapodhurika na matukio ya aina hiyo ni pigo kwa taifa katika midani ya kimataifa si unajua hawa watu wanakuja kutembelea mbuga zetu? tourism ikiadhirika uchumi wetu utayumba...
Kuhusu swala la ulinzi wa
obama hiyo ukiamua utafuta kauli mwenyewe,lakini kama hautojari unaweza
kutujuza juu ya hiyo dawa ya kukaushia maiti,ni kama hatari namna hii
unayojaribu kuonyesha mbona iko mikononi mwa watu wa ajabu sana? Wale
jamaa wa mochwari rushwa zao hazizidi hata elfu tano.
jamani,acheni kujifanya wataalam,hv maji makali ya betri ya gari mnayafahamu kwa kiasi gani?wala hayana madhara kwa kiasi hicho,mbona mngeyasikia mengi sana huko kwenye hzo gereji?au mnadhani kule hakuna maadui?hata siku moja mkemia mkuu hawezi kusema ni aina gani ya acid iliyotumika ktk uhalifu kwasababu za kiusalama zaidi.
.................,ni kwenye laborary zetu hizi mashuleni,ni kutoka kwa mkemia mkuu,au wapi? Na hasa matumizi yake zaidi ya huko laboratory ni yepi?........................
Mkuu mawazo yako yamekaa kishule zaidi, ni kama vile ulitegemea ziweko kwenye Laboratories za Chemistry au kwa mkemia mkuu pekee. Kule Laboratories za shule tunachanganya chemicals mbalimbali kama sehemu ya masomo yetu, lakini huku duniani hivyo vitu viko kwenye matumizi kama mahospitalini, viwandani na zingine kuuzwa maduka ya spare za magari na kutumiwa hata na wale ambao hizo Laboratory hawazijui.
Mfano mafundi wengi wa garage za magari wanazinunua hizo acid ''maji ya betri makali'' zinawekwa kwenye battery za magari kuongeza nguvu ya battery kuwasha injini ya gari. Hapa cha msingi ni matumizi tu ya hizo acid yamepindishwa kama ambavyo yanavyoweza pindishwa matumizi ya kitu kingine chochote.
Acid za kwenye berti za magari si kali kihivyo
maji ya betri hayana madhara sana juu ya ngozi though ni very dangerous internally,kama vile kwenye meno na kwenye utumbo.
kuna acid ni hatari na zina ulinzi mkali wa kimyakimya,ukiuliza tu,unadakwa.!labda iwe kimagendo kwani uadilifu hakuna kwa viongozi wetu.
sred klozd
Sio kukalili bali sikuelezwa.Hivyo unamaanisha tindikali inauzwa na watu hata wasio na utaalamu wa kuihandle? Hii inatofauti gani na hayo maduka kuuza silaha?
By the way tindikali inafanya nini kwenye betri ya gari?
Rihana ,rudi utetee hoja yako,betri za magari zina acidi sawa lakini sio acidi inayoweza kusababisha madhara kwenye ngozi kwa namna inayojurikana mpaka sasa.
Utaalamu wa nini wakati hapo imeuzwa kama maji ya betry, tindikali kwenye betri si ndio inasababisha betry iwe ina charge maana mfumo wa umeme wa gari unaendeshwa na betri hasa unapowasha na likishawaka wakati engine inazunguuka ina charge ile betry sasa humo kwenye betry kuna process inaendelea kuhusu hiyo acidi
Maji ya betry ni makali mkuu wewe just imagine ukivaa jeans tu kama betry limekugusa kidogo na pale ni unyevu tu baada ya muda inachanika, sasa sembuse maji yenyewe umwagiwe usoni mkuu, jaribu tu kuchua maji ya betry uone kazi yake ilivyo na ndio maana unaona hata hao waliomwagiwa acid wapo vile na kama ingekuwa acid unayoijua wewe nadhani ingewabandua mpaka minofu na kufa palepale (ngozi si ngumu kama tunavyodhani)
Ndugu yangu unaonekana una knowledge ndogo sana ya mambo... yale maji ya betri ndiyo yanaipa betri nguvu ya ku ignite engine...ni highly corrosive nenda dukani yanauzwa sh 3000 nunua halaf weka kwenye nguo uone ukali wake...sasa kama yanaweza kuyeyusha nguo je mtu akimwagiwa usoni inakuwaje? serikali haiwezi kudhibiti uuzaji wa acid ya gari kwa sababu matukio mengi ya kumwagia watu tindikali yanakuwa na motives fulani hata kisu nyumbani kinaweza kuwa silaha tu na kuuwa na huwezi kusema serikali idhibiti visu visiuzwe
I need to experiment this now.
Inawezekana kazi ya acid kwenye betri ikawa ni kuhifadhi charge?
kwani mbona ulishaeleza kuwa kuna aina kadhaa za acid,tena ulizitaja hadi majina,sulphuric acid,hydrochrolic acid,boric acid,nk,hzo ndizo tindikali zenyewe kijana,au ulitaka uone imeandikwa "Tindikali"pale juu ndo ujue kuwa ni tindikali?anyway,yule jamaa waliom-ponda ponda jana kwa vitu vyenye ncha kali vinavoruka hewani ndo anajua zaidi.
ndugu umeiwakilisha vizuri sanaMara ya mwisho kuiona hii kitu kwa macho yangu ni katikati ya mwaka 2001 nikiwa form six kwenye laboratory ya chemistry.Ikamwagika kwa bahati mbaya kwenye meza mle laboratory,fukuto lililotokea pale sio mchezo,meza ikaungua eneo hilo utadhani imechomwa moto,ukweli toka form two nilipoanza kuifahamu hii ilikuwa ndio chemical content pekee inayoogovya kwenye chemistry laborary,wakati huo mtu hata akigusa chupa yenye hyrodrogen peroxide anashtuka na kuruka tena kwa kelele mamaaaaaa anadhani ni concentrated acid
Toka mwaka 2001 sijawahi kuiona tena,nakumbuka ni colourless lakini pia nakumbuka ziko za aina nyingi kama hyrochloric acid,sulphuric acid,ethanoic acid,boric acid nakadharika lakini naamini zote zinatabia sawa sawa.
Pale mwanza miaka ya mwishoni mwa 1990 mbunge wa jimbo la mwanza kabla halijagawanywa baada ya ujio wa kijana masha alimwagiwa tindikali akiwa ofisini mwake,watu wanadai sababu ni kwamba alikuwa anatembea na wake za watu,namkumbuka kwa jina moja bwana shomari,kama ilivyokuja kuwa kawaida kwa upande wangu na yeye alimwagiwa kichwani lakini nadhani yule mtu alimwagia akiwa nyuma yake hivyo eneo kubwa lililoathiriwa ni shingoni.
Kiukweli,na hii inaweza ikawa ni moja ya tatizo la mfumo wetu wa elimu,mpaka leo dhaidi ya kukumbuka kwamba acids zinatumika kutengeneza chumvi sikumbuki matumizi mengine ya hii kemikali na bado naamini haitumiki kutengeneza chumvi hii tunayokula sababu inapatikana naturally (thanks God) kama pale uvinza.
Ni wazi matumizi mengine ni haya ya ugaidi ama kudhuru watu wengine,wakati ule bado mdogo hata mimi niliposikia mbunge wangu kamwagiwa tindikali sababu ya kukwiba wake za watu nilisema "size yake" lakini hivi sasa nimebadirika,sasa siamini hata kama ile ilikuwa ni sababu ya kweli,sasa naona njia sahihi nikuwafikisha watuhumiwa kwenye mikono ya sheria.
Niende kwenye hoja ya msingi,hawa watu wanaipata wapi tindikali,na naona lugha yetu imeipa jina mujarab (tindi-KALI),ni kwenye laborary zetu hizi mashuleni,ni kutoka kwa mkemia mkuu,au wapi? Na hasa matumizi yake zaidi ya huko laboratory ni yepi?viwanda gani vinatumia acid nchini,kuna matumizi yoyote ya kawaida yanayoweza yakamfanya muendesha bodaboda na yeye akawa nayo?