Mara ya mwisho kuiona hii kitu kwa macho yangu ni katikati ya mwaka 2001 nikiwa form six kwenye laboratory ya chemistry.Ikamwagika kwa bahati mbaya kwenye meza mle laboratory,fukuto lililotokea pale sio mchezo,meza ikaungua eneo hilo utadhani imechomwa moto,ukweli toka form two nilipoanza kuifahamu hii ilikuwa ndio chemical content pekee inayoogovya kwenye chemistry laborary,wakati huo mtu hata akigusa chupa yenye hyrodrogen peroxide anashtuka na kuruka tena kwa kelele mamaaaaaa anadhani ni concentrated acid
Toka mwaka 2001 sijawahi kuiona tena,nakumbuka ni colourless lakini pia nakumbuka ziko za aina nyingi kama hyrochloric acid,sulphuric acid,ethanoic acid,boric acid nakadharika lakini naamini zote zinatabia sawa sawa.
Pale mwanza miaka ya mwishoni mwa 1990 mbunge wa jimbo la mwanza kabla halijagawanywa baada ya ujio wa kijana masha alimwagiwa tindikali akiwa ofisini mwake,watu wanadai sababu ni kwamba alikuwa anatembea na wake za watu,namkumbuka kwa jina moja bwana shomari,kama ilivyokuja kuwa kawaida kwa upande wangu na yeye alimwagiwa kichwani lakini nadhani yule mtu alimwagia akiwa nyuma yake hivyo eneo kubwa lililoathiriwa ni shingoni.
Kiukweli,na hii inaweza ikawa ni moja ya tatizo la mfumo wetu wa elimu,mpaka leo dhaidi ya kukumbuka kwamba acids zinatumika kutengeneza chumvi sikumbuki matumizi mengine ya hii kemikali na bado naamini haitumiki kutengeneza chumvi hii tunayokula sababu inapatikana naturally (thanks God) kama pale uvinza.
Ni wazi matumizi mengine ni haya ya ugaidi ama kudhuru watu wengine,wakati ule bado mdogo hata mimi niliposikia mbunge wangu kamwagiwa tindikali sababu ya kukwiba wake za watu nilisema "size yake" lakini hivi sasa nimebadirika,sasa siamini hata kama ile ilikuwa ni sababu ya kweli,sasa naona njia sahihi nikuwafikisha watuhumiwa kwenye mikono ya sheria.
Niende kwenye hoja ya msingi,hawa watu wanaipata wapi tindikali,na naona lugha yetu imeipa jina mujarab (tindi-KALI),ni kwenye laborary zetu hizi mashuleni,ni kutoka kwa mkemia mkuu,au wapi? Na hasa matumizi yake zaidi ya huko laboratory ni yepi?viwanda gani vinatumia acid nchini,kuna matumizi yoyote ya kawaida yanayoweza yakamfanya muendesha bodaboda na yeye akawa nayo?