Timu za watoto wa kihuni

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,455
30,875
Orodha ya timu za mpira wa miguu za watoto wa kihuni pamoja na vituko vyao katika soka, premier league na mchangani, bila kusahau wana soka waliokuwa wanacheza soka la kihuni.

Mimi naanza na timu zangu...

1. NYOTA NYEKUNDU.
2. CONGO UNITED
3.SIFA UNITED watoto wa Tandale....
5. ASHANTI YA ILALA

4. Kuna watu wanaitaja na AFRICAN SPORT ya TANGA but sijalithibitisha hilo.


ONGEZA NYINGINE NA VITUKO VYAO KWENYE SOKA.




KISA KIMOJA : NYOTA NYEKUNDU walikuwa na beki wao anaitwa JOHN BOSCO ambae baadae alisajiliwa na Simba. Kabla hajasajiliwa Simba, Madaraka Suleiman mzee wa Kiminyio, alisajiliwa Majimaji ya Songea akitokea Sifa United ya Tandale.


Maji maji wakaja kucheza na Nyota Nyekundu uwanja wa taifa. John Bosco akawa ndo anamkaba Madaraka. John Bosco alimchezea sana rafu Madaraka, ila Madaraka akawa ana mkaushia tu. Kala sana vipepsi nakadhalika..

Game ilivyoisha Madaraka akamfuata John Bosco nje ya dimba. Akamwamkwida akimwambi:

" We msengwile unaniona mi fala eeh kwa sababu nachezea Majimaji? Unaniona mi mngoni?" John Bosco alichezea kichapo cha haja. Wachezaji wengine wa Nyota Nyekundu wakakaushia tu kwa sababu wanajuma madaraka mtoto wa SIFA UNITED ya Tandale na moto wa watoto wa SIFA UNITED walikuwa wanaujua."

Dondosha jina la timu yoyote iliyo kuwa inacheza mpira wa kihuni pamoja na vituko vyao.
 
ABAJALO kuna siku walienda kucheza Kwa wanajeshi sasa dogo mm akataka kuleta uhuni wao kwa wanajeshi
wanajeshi wakamdaka wakamwambia wewe unaleta uhuni wakataka kumshushia kipondo, dogo akajitetea kuwa amekuja kucheck MPIRA tu hivyo wamsamehe

basi wakamuuliza kuwa si umekuja kuona MPIRA tu ?

dogo kajibu ndio akafikiri watamuachia

wakamchukua mpaka mbali ya uwanja akawa hawezi ona game wanajeshi wakaleta MPIRA ule wa kuchezea wakauweka MPIRA ule mbele dogo wakamwambia akae, dogo akakaa halafu wakamwambia haya angalia MPIRA huo na ole wako uache kuuangalia
Huku game linaendelea

Dogo akaangalia ule MPIRA wa kuchezea dakika 90 zote huku kwenye uwanja timu zilivyomaliza kucheza wale wanajeshi wakamfuaata dogo wakachukua MPIRA wao halafu wakamwambia dogo apotee

DOGO alichomoka spidi 180
 
Ubatani na Macho kuvimba za Keko Mwanga na Machungwa.

Refa ana panga kiunoni na bangi Mtu. Ili mechi iishe salama matokeo yawe sare
 
Sheratoni na Mzizi
Hizitimu zilikua hasimu sana miaka ile 2000 kushuka chini

Nakumbuka zikicheza Tandika nzima ina simama.
Nakumbuka kila timu ilikua na watemi wake wa boxa.
Gemu ikiisha ni kupora tu Tandika nzima
 
Ngoma boom fc na ashanti amani inatawala game ikipigiwa air wing ila tatizo wakitoka huko ile nginjanginja mpaka baharini asiombe kukutana nao.

Mechi zao refa anapulizia kipenga getini. Jamaa walikua wanaenda na mapanga, fimbo mawe, n.k. km vile kwa Madiba wanavyoenda na Vuvuzela.....

ASHANTI na BOM BOM.... balaa kubwa
 
Game la Blackpool ya Vingunguti Vs Karakata Fc ya Airport uwanja wa Karume , dk 20 za mwanzo Blackpool wanapata goli, mashabiki wao wa jukwaa kuu wote wamenyanyua mapanga ndani ya sekunde kadhaa kama ishara ya kusherehekea, game liliisha 1-1
 
Huku mbagala kuna timu ilikua inaitwa stombagi na nyingine kapet.. Hzo timu samata mwenyew alikua hapati namba.. Mana humo mpira ni rafu kwenda mbele.. Nilishuhudia mara mbili mtu akivunjwa mguu.. Refa ni pusha maarufu wa bhangi wkumuita stiga... Mkononi ana pisi la bangi kiunoni ana panga..
Alikua hatoi kadi yeye ukicheza rafu unapewa konzi unatulia mana anaye pia alikua mbabe..
Ili mpira uishe salama matokeo lazima yawe sare..
 
Huku mbagala kuna timu ilikua inaitwa stombagi na nyingine kapet.. Hzo timu samata mwenyew alikua hapati namba.. Mana humo mpira ni rafu kwenda mbele.. Nilishuhudia mara mbili mtu akivunjwa mguu.. Refa ni pusha maarufu wa bhangi wkumuita stiga... Mkononi ana pisi la bangi kiunoni ana panga..
Alikua hatoi kadi yeye ukicheza rafu unapewa konzi unatulia mana anaye pia alikua mbabe..
Ili mpira uishe salama matokeo lazima yawe sare..

Da hiyo ni nouma sana halafu kama ni mechi ya mtoano timu ya wababe ikifungwa, refa hakuna kumaliza mpira mpaka wababe wasawazishe
 
Back
Top Bottom