Timu za Congo DRC Klabu Bingwa Afrika msimu huu hamna kitu

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Vita uji, TP Mazembe mtori, watu wanajinywea tu, wanatakiwa kutuliza vichwa wajenge upya vikosi vyao.

Vita kupata draw away kwa Al Ahly kumbe ilikuwa ni bahati tu, walitakiwa kufa sio chini ya goli nne ni vile tu washambuliaji wa Ahly hawakuwa makini, leo Vita katandikwa nyumbani kwake na muarabu 3-0.

Hao Mazembe nao mbele ya Mamelodi Sundowns hawana chao, wanahitaji muujiza kushinda away kwa wale wasauz wanaopiga mpira kama hawana akili nzuri, nionavyo viwango vya hizi timu mbili za Congo vimeanza kushuka.
 
Sawa ila mazembe atapita
Hili kundi kashinda mmoja tu game zote nne
Screenshot_20210316-204442.jpg
 
Kuna mdau alishasema humu kwamba,msimu huu hawajasajili, As Vita wana ukarabati mkubwa wa uwanja wao,vilevile waliuza sana wachazaji wao. Tp Mazembe nao wana project kubwa pia msinu huu wamepromote wachezaji vijana ila msimu ujao watakuwa moto.
 
Nilisikia mahojiano fulani kutoka Congo kabla ya mechi hii bt nimesahau chanzo ila nakumbuka fact...ni kwamba kwa TP Mazembe Katumbi ameshusha budget ya timu kutoka milioni 10 kwa wiki kufikia milioni 5...pia wamekuwa wakisajili wachezaji ambao ni average hata wakutoka nje ya nchi na hivyo timu kushuka kiuwezo.
 
Hapa kuna neno, nikimkumbuka yule wa Mbeya City jina nimelisahau kidogo, na Singano naona kuna point hapo.
 
Kuna mdau alishasema humu kwamba,msimu huu hawajasajili, As Vita wana ukarabati mkubwa wa uwanja wao,vilevile waliuza sana wachazaji wao. Tp Mazembe nao wana project kubwa pia msinu huu wamepromote wachezaji vijana ila msimu ujao watakuwa moto.
Ni kweli lkn sio sababu sana,cz hao al ahly pia wana pjrct ya viwanja vya michezo tena hicho kituo hadhi ya Olympic

Hizo timu zimeuza wachezaji wazuri wamenunua underground ,mfn Mazembe toka wauze, Ben malango,Jackson muleka,Meshack Elia hawajanunua mchezaji mzuri zaidi ,ya baleke,dje dje ,beya
 
Nilisikia mahojiano fulani kutoka Congo kabla ya mechi hii bt nimesahau chanzo ila nakumbuka fact...ni kwamba kwa TP Mazembe Katumbi ameshusha budget ya timu kutoka milioni 10 kwa wiki kufikia milioni 5...pia wamekuwa wakisajili wachezaji ambao ni average hata wakutoka nje ya nchi na hivyo timu kushuka kiuwezo.
Sawa sawa budget imeshuka imesajiri wachezaji wa kawaida Sana, djedje,baleke,tshibangu,beya ,kifupi lescobeaux /Mazembe na black dolphins/Vclubien hawana timu nzuri msimu huu

Katumbi kapunguza budget
Gen Tango four Siku hz hayuko na Vclubien km zamani ,timu iko kwa Madame
 
Nilisikia mahojiano fulani kutoka Congo kabla ya mechi hii bt nimesahau chanzo ila nakumbuka fact...ni kwamba kwa TP Mazembe Katumbi ameshusha budget ya timu kutoka milioni 10 kwa wiki kufikia milioni 5...pia wamekuwa wakisajili wachezaji ambao ni average hata wakutoka nje ya nchi na hivyo timu kushuka kiuwezo.
Kweli wasingeweza kusajili wachezaji kiwango cha Singano na Atupele! kwa namna ilivyokuwa TP Mazembe
 
Vita uji, TP Mazembe mtori, watu wanajinywea tu, wanatakiwa kutuliza vichwa wajenge upya vikosi vyao.

Vita kupata draw away kwa Al Ahly kumbe ilikuwa ni bahati tu, walitakiwa kufa sio chini ya goli nne ni vile tu washambuliaji wa Ahly hawakuwa makini, leo Vita katandikwa nyumbani kwake na muarabu 3-0.

Hao Mazembe nao mbele ya Mamelodi Sundowns hawana chao, wanahitaji muujiza kushinda away kwa wale wasauz wanaopiga mpira kama hawana akili nzuri, nionavyo viwango vya hizi timu mbili za Congo vimeanza kushuka.

Al ahly na Wydad Casablanca is my favourite team. Mmoja wao lazima abebe kombe hili, mnyama i know that hana chake.
 
Back
Top Bottom