py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,471
- 4,424
TIMU ZA N.AFRICA ZITAENDELEA KUTAWALA
-Ukizungumzia soka la bara la Africa Maarufu kama CAF champions league lazima utagusa ukanda wa Afrika kaskazini sababu klabu kutoka ukanda huo wamekuwa wakitawala michuano haya kwa muda mrefu wakipata changamoto kwa vilabu 2 tu ambazo ni TP Mazembe kutoka DRC na mamelody kutoka Afrika kusini .Nini siri ya vilabu hivi kutesa soka la bara ka Afrika
1.Wydad Casablanca
2.Al Ahly
3.Es Setif
4.Esperance de tunis
5.Etoel du sahel
6.USM Alger
7.Mc Alger
Vilabu hivi ama magwiji hawa wamekuwa wakifika nusu fainali ya CAF kila wakati na kuchukua makombe na vilabu kutoka ukanda mwingine ni Mazembe na Mamelody Sundowns tu ndio wamekuwa wakiwapa changamoto vinara hawa kutoka Afrika kaskazini
Kuna watu wanasema vilabu vya Afrika kaskazini wakiwaita kwa jina maarufu "waarabu" kuwa wana fitina la hasha sio kweli nimewafuatilia sana
1.Licha ya timu hizi kucheza soka la kuvutia lakini silaha yao kubwa ni mashabiki ,ukienda away kucheza na vilabu hivi tegemea kufungwa magoli mengi kuanzia 4-na kuendelea.
2.Mashabiki kuanzia dakika ya 1-90 wanashangilia kwa nguvu ,makelele ,wanawasha moto mekundu ,wanapiga ngoma kwa nguvu na spirit ya wachezaji inakuwa juu sana nawapa assignment tafuta matokeo ya nyumbani ya vilabu niliyoorodhesha hapo juu utaona wanashinda 9,7,6
2.Turudi bongo nilikuwa natizama game ya yanga na Township rollers la haula uwanja ulikuwa na ma gap mengi ,mapengo mengi na pia hao mashabiki waliokuwepo wanashangilia kwa matukio haswa kwenye mashambulizi ya kustukiza au kanzu tobo ila muda mwingi wapo kimya kama maiti mpaka unajiuliza mantiki ya mashabiki kwenda uwanjani ni nini sasa ukiwa kimya muda mwingi mpaka goli liingie huko sio kuiunga timu na kuipa nguvu
Hebu vilabu vyetu pendwa simba na yanga igeni mfano kutoka Al ahly hapo chini au WAC Casablanca hapo juu ,mnavyoona timu zinapigwa goli 5,6,7 huko kwao na kufika fainali kila mwaka sio wanajua sana ila makelele ,pressure ya mashabiki huchangia kwa kiasi kikubwa na hakuna fitna yeyote.
Au tizama Al Ahly walivyocheza na yanga mpaka yanga wakapoteana uwanjani walishindwa kuendana na presha
NB:Mashabiki wa simba na yanga msiwe maiti uwanjani badilikeni