Wana jamvi kuna taarifa kuwa timu kabambe ya ukawa inayo undwa na wabunge wote wa chadema,cuf na nccr waliopo bungeni kuanzia ijuu ijayo kuanza ziara ya siku 21 mikoani,wataongozwa na kamanda mbowe kwa pamoja na james mbatia watatumia magari na chopa kuongeza nguvu ukanda wa kwanza kushambuliwa utakua ukanda wa pwani na morogoro;ratiba kamili itatolewa muda mfupi ujao;taarifa hizi ni tetec ya muda mfupi kabla ya ratiba kuwekwa hadharani
Hata wangeamua kuahirisha kabisa bunge, ili kwenda kutoa elimu kwa Wananchi, mimi ningeunga mkono hilo. Naona kuna wanaofikiria
"hii ni kukosa uzalendo....huyu ni....#**^%@$... kabisa"!. Kabla mtu hajatamka hayo "mawazo" kwa sauti nitoe sababu za kuona hivyo:
1. Nadhani swala la katiba ni la muhimu kwa nchi kuliko hata bajeti, kwani ni kutokana na uhuru na ubovu ambao CCM imeupata kutoka kwenye katiba ya sasa, ndiyo maana tumekuwa tukipata bajeti mbovu, zisizotekelezaka kwa miaka kibao. Pia sioni kama hata mchango wa upinzani katika katiba kama unathaminiwa, kwani ni kawaida kwamba pamoja na bajeti kuwa mbovu, na wabunge wa upinzani kuzikosoa kwa vielelezo, bado zimekuwa zikipitishwa kwa sababu ya wingi wa wabunge wa CCM, wasiojali maslahi ya nchi.
2. Wananchi wamekuwa wakiburuzwa kwa muda mrefu, kwa sababu ya elimu duni, hasa ya uraia. Wamekuwa hawajui ukweli wa mambo mengi, hasa tangu kuanzishwa kwa taifa hili kwa hiyo wamejikuta wanafuata mkumbo usio sahihi. Mpaka sasa wanadhani serikali inawajali kwa sababu imewajengea shule. Wanashindwa hata kumalizia kufikiria walimu wako wapi, kwa nini hakuna maabara, inakuwaje hakuna maktaba? Hili ni tatizo! Kwamba wameshindwa kustuka kuwa kujengewa majengo bila malengo ni matumizi mabaya ya fedha! Kwamba wao wanaimba nyimbo za kuitukuza CCM kwa kujenga barabara. Wanashindwa hata kustuka kwa nini kuna barabara zilijengwa tangu awamu ya kwanza na zipo, halafu kuna barabara zimejengwa mwaka jana leo zimechoka na zina viraka hakuna mfano! Hili ni tatizo kubwa. Leo wanachi wanaimba nyimbo za kisiasa za "uchumi unakuwa kwa kunapaa" wanashindwa hata kustuka miaka ya nyuma kulikuwa na bidii ya kudhibiti bei za vitu, sasa kila mtu ana uhuru wa kujipangia bei, na bidhaa zimekuwa hazinunuliki tena mpaka wanakula mlo mmoja kwa siku. Uchumi gani unakua wakati shilingi inashuka thamani kila mwaka?
Mimi nadhani wananchi hawa wanahitaji elimu kuliko kitu chochote kwa sasa. Waambieni hao jamaa wawahi huko, ikibidi hata bungeni watoke kwa nia nzuri tu (siyo ya kususa chochote) kwani wananchi wanhita msaada wao. Bajeti itapitishwa na CCM kama kawaida. Kwani hata wakikaa, wakapinga wakakosoa si ni wazi kuwa bado itapita? Watoe mchango kwa maandishi wakati wanaelimisha Watanzania!