Timu ya UKAWA iliyopo bungeni kuanza ziara mikoani wiki ijayo

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
887
0
Wanajamvi,

Kuna taarifa kuwa timu kabambe ya UKAWA inayoundwa na wabunge wote wa CHADEMA,CUF na NCCR Mageuzi waliopo bungeni kuanzia ijumaa ijayo kuanza ziara ya siku 21 mikoani.

Wataongozwa na kamanda Mbowe kwa pamoja na James Mbatia.

Watatumia magari na chopa kuongeza nguvu ukanda wa kwanza kushambuliwa utakua ukanda wa Pwani na Morogoro.

Ratiba kamili itatolewa muda mfupi ujao.

Taarifa hizi ni tetesi ya muda mfupi kabla ya ratiba kuwekwa hadharani.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Wana jamvi kuna taarifa kuwa timu kabambe ya ukawa inayo undwa na wabunge wote wa chadema,cuf na nccr waliopo bungeni kuanzia ijuu ijayo kuanza ziara ya siku 21 mikoani,wataongozwa na kamanda mbowe kwa pamoja na james mbatia watatumia magari na chopa kuongeza nguvu ukanda wa kwanza kushambuliwa utakua ukanda wa pwani na morogoro;ratiba kamili itatolewa muda mfupi ujao;taarifa hizi ni tetec ya muda mfupi kabla ya ratiba kuwekwa hadharani

Hata wangeamua kuahirisha kabisa bunge, ili kwenda kutoa elimu kwa Wananchi, mimi ningeunga mkono hilo. Naona kuna wanaofikiria "hii ni kukosa uzalendo....huyu ni....#**^%@$... kabisa"!. Kabla mtu hajatamka hayo "mawazo" kwa sauti nitoe sababu za kuona hivyo:

1. Nadhani swala la katiba ni la muhimu kwa nchi kuliko hata bajeti, kwani ni kutokana na uhuru na ubovu ambao CCM imeupata kutoka kwenye katiba ya sasa, ndiyo maana tumekuwa tukipata bajeti mbovu, zisizotekelezaka kwa miaka kibao. Pia sioni kama hata mchango wa upinzani katika katiba kama unathaminiwa, kwani ni kawaida kwamba pamoja na bajeti kuwa mbovu, na wabunge wa upinzani kuzikosoa kwa vielelezo, bado zimekuwa zikipitishwa kwa sababu ya wingi wa wabunge wa CCM, wasiojali maslahi ya nchi.

2. Wananchi wamekuwa wakiburuzwa kwa muda mrefu, kwa sababu ya elimu duni, hasa ya uraia. Wamekuwa hawajui ukweli wa mambo mengi, hasa tangu kuanzishwa kwa taifa hili kwa hiyo wamejikuta wanafuata mkumbo usio sahihi. Mpaka sasa wanadhani serikali inawajali kwa sababu imewajengea shule. Wanashindwa hata kumalizia kufikiria walimu wako wapi, kwa nini hakuna maabara, inakuwaje hakuna maktaba? Hili ni tatizo! Kwamba wameshindwa kustuka kuwa kujengewa majengo bila malengo ni matumizi mabaya ya fedha! Kwamba wao wanaimba nyimbo za kuitukuza CCM kwa kujenga barabara. Wanashindwa hata kustuka kwa nini kuna barabara zilijengwa tangu awamu ya kwanza na zipo, halafu kuna barabara zimejengwa mwaka jana leo zimechoka na zina viraka hakuna mfano! Hili ni tatizo kubwa. Leo wanachi wanaimba nyimbo za kisiasa za "uchumi unakuwa kwa kunapaa" wanashindwa hata kustuka miaka ya nyuma kulikuwa na bidii ya kudhibiti bei za vitu, sasa kila mtu ana uhuru wa kujipangia bei, na bidhaa zimekuwa hazinunuliki tena mpaka wanakula mlo mmoja kwa siku. Uchumi gani unakua wakati shilingi inashuka thamani kila mwaka?

Mimi nadhani wananchi hawa wanahitaji elimu kuliko kitu chochote kwa sasa. Waambieni hao jamaa wawahi huko, ikibidi hata bungeni watoke kwa nia nzuri tu (siyo ya kususa chochote) kwani wananchi wanhita msaada wao. Bajeti itapitishwa na CCM kama kawaida. Kwani hata wakikaa, wakapinga wakakosoa si ni wazi kuwa bado itapita? Watoe mchango kwa maandishi wakati wanaelimisha Watanzania!
 
sir joshua

JF-Expert Member
May 21, 2013
480
225
tehe tehe taratibu ukawa watu wanazimia kwa kihoro huku mitaan,nepi na kinena lazama pichu ziruke
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,491
2,000
Tunawakaribisha kwa mikono miwili karibuni.

Sipati picha itakuwaje kwani hawa waliopo tu kwenye hizi ziara lipumba na slaa hali mbaya sasa hiyo timu ikijakushuka yote (the dream tyme) si mgambo (magamba) wataruka na kukanyagana!!! Jana tu nimemuona dr.balali huko japan anawaomba diaspora wawabembeleze ukawa warudi bungeni, hadi anatia huruma.
 
JAKOBO

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
934
0
Nami nipo kwenye bus natokea Dar nakonga mioyo yawatanganyika kwa kuitangaza vyema UKAWA na mwitikio nimkubwa Sana abiria wote wananiunga mkono nakunisikiliza kwa makini.Nisingependa kutaja mahali nilipofika na bus niliyomo kwa sbb za usalama wangu na abiria mana Ccm wapo radhi hata kuangusha bus mfe wote kama wakigundua kwamba tunapiga kote mpaka kwenye vyombo vyausafiri!!
Wadau mniombee safari iwe salama nisikutane na interahamwe
 
Nnangale

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,873

Mkuu safari njema mola atakulinda
 
manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
Nami nipo kwenye bus natokea Dar nakonga mioyo yawatanganyika kwa kuitangaza vyema UKAWA na mwitikio nimkubwa Sana abiria wote wananiunga mkono nakunisikiliza kwa makini.Nisingependa kutaja mahali nilipofika na bus niliyomo kwa sbb za usalama wangu na abiria mana Ccm wapo radhi hata kuangusha bus mfe wote kama wakigundua kwamba tunapiga kote mpaka kwenye vyombo vyausafiri!!
Wadau mniombee safari iwe salama nisikutane na interahamwe

ha ha ha nimecheka sana loh ....!!!acha uoga ha ha
 
Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,296
0
Nami nipo kwenye bus natokea Dar nakonga mioyo yawatanganyika kwa kuitangaza vyema UKAWA na mwitikio nimkubwa Sana abiria wote wananiunga mkono nakunisikiliza kwa makini.Nisingependa kutaja mahali nilipofika na bus niliyomo kwa sbb za usalama wangu na abiria mana Ccm wapo radhi hata kuangusha bus mfe wote kama wakigundua kwamba tunapiga kote mpaka kwenye vyombo vyausafiri!!
Wadau mniombee safari iwe salama nisikutane na interahamwe

Ha ha duh hadi raha afar njema bwana wakoleze na injili ya UKAWA
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Sipati picha itakuwaje kwani hawa waliopo tu kwenye hizi ziara lipumba na slaa hali mbaya sasa hiyo timu ikijakushuka yote (the dream tyme) si mgambo (magamba) wataruka na kukanyagana!!! Jana tu nimemuona dr.balali huko japan anawaomba diaspora wawabembeleze ukawa warudi bungeni, hadi anatia huruma.

Hawaeleweki mara Katiba mpya haiitajiki mara serikali mbili tu,hata sijui,isije ikawa ndiyo U-Banda umeshawasili,ukishindwa kwenye uchaguzi,vunja uchaguzi tangaza mwingine.Ukubwa raha.Mambo ya chama tawala hayo kaka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom