PreGE2025 Timu ya Kampeni ya 'Mama Asemewe' watinga mtaani kumsemea Rais Samia

PreGE2025 Timu ya Kampeni ya 'Mama Asemewe' watinga mtaani kumsemea Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kikubwa ni kuwakariri tu, hakuna marefu yasio na ncha. Zama hizi zitapita wakija wenye akili tutafanya kuwaumbua tu.
 
Hawa Chawa hawawezi kujibu HOJA za CHADEMA na ACT WAZALENDO za kwamba mfumo wa Uchaguzi hauko FAIR wala HURU unawapendelea CCM haufuati matakwa ya Watanzania.
Mambo ya Uchaguzi sio kipaombele Cha Umma Bali maendeleo
 
Wamefika wapi hawa? Tuwaambie ukandamizaji tunaofanyiwa wananchi huku mtaani toka kwa watendaji wa hovyo wakampelekee.
 
Katika kuadhimisha Wiki ya Mama, Timu ya Kampeni ya Mama Asemewe imefanya ziara katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo wameeleza umuhimu wa kuchagua viongozi bora kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 pamoja na kuonyesha kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Timu hiyo, ikiongozwa na Bw. John Danda Katibu mkuu wa Samia for Us, Makamu Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Bi. Verynance Mrema na Anna Kivuyo, Naibu Katibu Mkuu wa Samia for Us, imewahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kuwalekeza juu ya mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia katika kipindi cha miaka minne madarakani.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 20 Machi 2025, wananchi walielezwa kuhusu miradi ya maendeleo, juhudi za kuboresha huduma za jamii, na mchango mkubwa wa Rais Samia katika kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, wananchi walieleza kuridhika kwao na mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali, kama vile elimu, afya, miundombinu, na uchumi, katika kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wananchi wameonesha shukrani zao kwa Serikali kwa hatua zinazochukuliwa katika kuboresha maisha yao na ustawi wa taifa.

Aidha Ziara hiyo imejikita katika kuhamasisha wananchi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu kuchagua ongozi bora na umuhimu wa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukuza maendeleo ya taifa.

Kikundi hicho kimesajiliwa? Mbona polisi hawawakamati kama wale jamaa wa NETO?
 
Vijana wa namna hii katika nchi ni hatari sana.

Hivi kampeni zimeanza?

Hakuna anayetaka kufanya vurugu au kuzuia uchaguzi, kinachotakiwa ni "fair and free election"

Wazee huko CCM waambieni hawa vijana Taifa linahitaji vijana shupavu wenye kusimamia Taifa lao sio kupigania watu, Taifa linahitaji vijana wakupigania maslahi ya Taifa na watu wake na sio maslahi ya chama na wagombea nyadhifa.

CCM muache kuifanya siasa ndio ajira Kwa vijana, tunahitaji hii nguvu kazi kwenye kujenga nchi na sio kupiga blah blah mitaani.
Vijana wahivi wanapaswa kukuza upeo wao maana ukiwasikiliza tu unaoa na kugundua vichwa vyao NI empty.
 
Vijana waCDM Kesho wakianza kupitia nao mtaani na kuwaambia watu wasimchague mama maana Kwa sababu A,B,C,D nao mtawaacha.

Hawa vijana hawaoni kama kitendo cha kuachwa kupiga kampeni ndio tunasema hakuna fair and free election maana CCM inafanya kampeni na Tume ya uchaguzi imebaki inaangalia tu.
 
Back
Top Bottom