Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 766
- 1,536
Wakati mmojawapo ambapo utakutana na VIPANGAMIZI na upinzani mkubwa sana kwenye maisha yako ni pale UNAPOANZA kubadilisha viwango. Kama vile ambavyo ndege inatumia nguvu kubwa inapoacha ardhi na kuanza kupaa ndivyo hivyo hivyo na wewe.
Ukiwa hauna mbele wala nyuma hakuna tatizo, ukiwa unafanya mambo kwa mazoea hakuna tatizo, ukiwa unaongoza kwa kawaida tu na hakuna makubwa unayofanya hakuna tatizo, ukiwa unafanya kila mtu anachofanya hakuna tatizo, ukiwa una mawazo madogomadogo hakuna shida n.k
Changamoto itaanza pale unapotaka kuonyesha bidii zaidi ya ilivyozoeleka, pale unapotaka kuonyesha uaminifu ukiwa umezungukwa na watu wasio waaminifu, pale unapoonyesha moyo wa kutetea wanyonge katikati ya wanaofurahia kuwakandamiza, pale unaposema unataka kuishi ndoto zako katikati ya watu waliokata tamaa kuhusu za kwao, hapo ndipo tatizo huanzia. Wengi watasema UNATAKA KUJIONYESHA, UNAJIPENDEKEZA, UNA NIA MAKUU ama UNAJIDAI.
Kuna watu wameinuka kukupinga sio kwa sababu nyingine yoyote ile bali ni kwa sababu UMEINUA KIWANGO. Kumbuka watu wengi wanafurahia wewe ukiwa kama wao, mara utakapoanza kuwa TOFAUTI tu unaanza kugeuka kuwa ADUI YAO. Kuna vitu walizoea kufanya, ukileta UTARATIBU tofauti wanaanza kukupiga VITA.
UPINZANI wa namna hii hautaisha kwenye maisha yako hadi unaondoka duniani. Usihangaike KURUDI KIWANGO cha chini ili KUFANANA NAO, endelea kupandisha viwango hadi utakapowaacha mbali sana kiwango ambacho KELELE ZAO hazitakuwa na athari kwako, kama vile ambavyo kelele za ANAYETEMBEA kwa MIGUU, hazimsumbui RUBANI wa ndege ALIYE JUU.
Uko tayari kuendelea KUKABILIANA NA UPINZANI wa NAMNA HII bila KUSHUSHA KIWANGO?
#Nanauka