Masalange; Kero ya usafiri katika mabasi iliyofumbiwa macho

Latebloomer

New Member
Oct 6, 2021
4
6
MASALANGE; KERO YA USAFIRI KATIKA MABASI ILIYO FUMBIWA MACHO!

Masalange au kama wanavyo penda kuitwa, Maafisa usafirishaji kwa kimombo " BUS AGENTS" ni watu ambao wamekuwepo katika kila Stendi za mabasi ili kurahisisha upatikanaji wa usafiri kwa abiria waendao maeneo mbali mbali nchini na nje ya nchi.

Masalange huwasaidia wateja kuwapeleka hadi sehemu ya kukatia tiketi na haswa kwa abiria ambao si mwenyeji au hawana uzoefu wowote wa masuala ya usafiri. Masalange hupinga vikali kuitwa WAPIGA DEBE ingawa kiuhalisia ndivyo. Pamoja na faida zote za urahisishaji kwa abiria, watu hawa wamekua kero na karaha katika usafiri wa mabasi kwa muda mrefu sasa.

Kuna abiria mmoja alisikika akisema " lina pokuja suala la kusafiri, huwa napata "head ache" pindi tu nikikumbuka kuna wale watu ( masalange) stendi. Ole wake mtu awe na Mzigo(mi-) basi kazi itamkuta na bahati mbaya kama ni mama Mfyele( mwenye mtoto au watoto wadogo) basi hapo ndio huwa patashika.

Watu hawa wamekua chanzo cha watu kusafiri katika mabasi kinyume na matarajio yao kwani akisha kukamata atakupeleka sehemu ambayo anaitaka alimradi tu apate Kamisheni hata kama basi ni bovu kupindukia. Watu hawa ni wajanja wa mali kauli wamejaa swaga za ulaghai mdomoni kwasababu unaweza kuwa umepanga kupanda basi flani lakini wakakulaghai na ukajikuta upo katika basi ambalo hukulitegemea.

Kuna watu wanaweza kuhisi kuwa ni uzembe wa wateja wa mabasi lahasha! niwahakikishie kwamba si kila mtu anaweza kuhimili mikiki ya hawa watu, kwanza ni wengi na ni mijitu iliyoshiba na ina makelele yakutosha. Kabla gari haija fungua mlango abiria watelemke wao ndio kwanza huziba mlango kwa kugombania abiria.

Mamlaka za usafiri zimetoa muongozo wa viwango vya nauli kwa abiria kulingana na umbali au jiographia, ubora wa miundombinu na aina ya chombo cha usafiri lakini chakushangaza Masalange hawa wanaongeza gharama zisizo na tija yoyote.

Mfano kumekua na suala la Ufaulishaji wa abaria ambapo abiria mfano wa Dodoma kwenda Mbeya nauli ya basi kubwa ni Tsh. 28000 analipa hiyo hela baadae akifika Iringa mfano ana Faulishwa kwenye Coaster na ilihali bei za Coaster zina julikana. kipindi cha usafiri kuwa adimu hasa wakati wa kufunga au ufunguzi wa shule na vyuo bei zimekua zikiongezeka kiholela holela tu kama vile hakuna mamlaka wajibifu.

Kesi za kuuziwa ticketi na baadaye ukakosa siti hadi leo tunaendelea kuzishuhudia. Very sad!

MTIZAMO WANGU:
Watu hawa wamekua kero na bughudha sana kwenye sekta ya usafiri na haswa kwa abiria. Serikali na mamlaka zinazo husika zitafute namna ya kuondoa kero hii ikiwemo kuwaondoa au kuwapunguza watu hawa . Naamini serikali ikiamua inaweza, tumeona mfano suala mifuko ya plastiki au rambo halikadhalika Viroba na sasa wamachinga.

Nikweli watu hawa wamejenga na wana tegemewa na familia zao lakini ifikie wakati kusurvive kupitia jasho la wanyonge haikubaliki.

Teknolojia nayo imekua na kwenda kasi sana. Tanzania ya leo sio Tanzania ya miaka ya 1980's. Kuna baadhi ya vitu hatuna budi kuku bali kuwa vimepitwa na wakati na kuviacha kama suala la Masalange. Hivi karibuni kuna watu walijaribu kupromote mfumo wa kielekroniki "Online bus ticketing". Si jajua so far umfumo huu umefikia wapi, ingawa moja kati ya changamoto yake ilikua ni kukwamishwa na hao hao masalange pamoja na Middlemen.

Mfumo huu wa kisasa ambao ni Artificial Intelligence au akili bandia kupitia "Online bus ticketing" ni rahisi na utaepusha usumbufu mwingi unao sababishwa na masalange kwa sasa. Artificial intelligence tayari imesha athiri watu wengi duniani na si kwamba hao masalange watakua watu wa kwanza lakini lengo nikutengeneza mazingira mwafaka na rafiki kwa wasafiri.

Pia kama ni wasi wasi wa kukosa abiria kwa upande wa wamiliki, mfumo mpya wa kisasa utawafanya walazimike kufanya promosheni za vyombo vyao vya usafiri kama wafanyavyo wafanya biashara wengine, na hii nafikiri itasiaidia hata wamiliki wa vyombo hivyo kuboresha miundo mbinu yao ili kuongeza ushindani. Kwa sasa ni ngumu kuboresha sababu wana uhakika hawa watu wao wataleta tu wateja hata kwa ujanja ujanja
By Mwambasi

Mwambasitumsifie@gmail.com
 
IMG-20220103-WA0015.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom