Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,479
- 5,224
Sasa kiranja mkuu, kwa nini usiwakamatishe kwa jamaa wa takukuru? maana inatia hasira sana unadhani mtu ameshinda kumbe ni usanii tu.... yaani umpe laki tisa na nusu? mmhh aisee ingekuwa ni mimi ningekubali baada ya kutanganza kuwa ni mshindi simpi hata sent tano kiushenzi ili next time hakome kufanya huo uchafu wao!Mimi nilisha fuatwa mara kadhaa na kuwadi wa hao watu wa i.t, nishiriki lile shindano la milioni moja,
nikichukua hiyo milioni moja nimpehuyo kuwadi laki tisa unusu kisha mi nibaki na hamsini elfu,
nikasema sifanyi dhuluma. Wapeni wanaostahili.
Ikatokea bahati nasibu ya kugombea tv na dish, nikafuatwa nikakataaa.
Leo kaja tena dalali mwingine, anasema wanipe line mpya kisha wanipigie kuwa nimeshinda shilingi millioni mbili.
Nimegoma nimewaambia kuwa mie sio dhulumati...
Wakatafute wahuni kariakoo wawape dili
Hii mii naunga mkono kuwa zawadi za tiGO ni feki.
Kuna jamaa yangu ambaye ana mama yake mdogo anafanya kazi tiGO, aliwahi kupigiwa simu wakati ule tiGO wanatoa zawadi za milioni moja. Mama yake alimwambia anunue vocha ya TZS 10,000 halafu atume ujumbe mara nyingi mpaka hiyo pesa iiishe, halafu yeye atajua jinsi ya kuseti kule tiGO. Aiseee, baada ya muda yule kijana akapigiwa simu kuwa ameshinda milioni moja ya tiGO. Tangu siku hiyo nikiona tiGO wanatangaza zawadi inanijia hisia ya mchezo huo mchafu.
Kweli kama IT wa tiGO wanafanya hivyo waache mara moja.
Kweli imani imekwisha.
Hivi hao wakulu wa kitengo hicho cha I.T kwani hawaijui michezo hii michafu?
Wanaijua, ila wananufaika nayo.
Maaana haiwezekani vijana wakawa wanacheza rafu, halafu mabosi wao wasijue.