TIGO-PESA Wameniibia manunuzi yaLUKU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TIGO-PESA Wameniibia manunuzi yaLUKU

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchukiaufisadi, Jan 12, 2012.

 1. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu nimeibiwa Tshs. 10,000 na Tigo-Pesa. Nilitaka kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Tigo-pesa. Nikafuata taratibu zote wakanipa na reference number. Baada hapo sikupokea chochote. Nimejaribu kuwa pigia kwa 0713800800 majibu ya muhudumu ni mabaya mno, kwa ukali akanijibu piga 150. Nimekuwa nikipiga 150 inaita haipokelewi kwa zaidd ya dakika 15 zaidi ya mara 7 toka juzi.

  Naomba msaada wa nini cha kufanya nikomboe pesa zangu. Kwenda ofisini kwao itakuwa ni sawa na hasara maana mafuta ni zaidi ya lita 7.

  Please help
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  mkuu dawa yao ni kutinga kwenye ofc zao ila kama umeona hailipi after cost benefit analysis endelea kuwasumbua kwa njia hiyo hiyo ikibidi tumia namba tofauti tofauti mpaka watatue! Wasikuzingue maisha magumu ati!
   
 3. A

  Ados Senior Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tunza sana hiyo referance namba yako usiwe na wasiwasi hela yako ipo haijapotea kama upo dar nenda ofisi za tigo za mlimani city au mtaa wa Ohio au K'koo kituo cha Gold Star
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tigo ni wezi hapana maelezo,nimekwenda kwa wakala kutoa pesa laki mbili,cha ajabu kwangu itoka haikunipa majibu kama imetoka ila imehama na kwa wakala haijafika, ninasumbuana nao leo siku ya tatu,custorme care wanamajibu mabovu sijapata kuona nikiwa kwenye ofisi zao mlimani city anakuja mama mwingine mwenye tatizo kama langu yeye ni elfu 40,wanamuwakia kisha wakampigia wakala na kutoa hela kwenye akaunti ya wakala kwa nguvu ghafra wakala anakuja na hasira akiwambi mmezidi kunitia hasara sikubali hii ni pesa yangu si ya tigo nataka pesa yangu.mambo ni vurugu tu na wizi kwa kwenda mbele
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Itabidi tususie huduma zao.
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  mi wameshaniibia mara mbili,mijambazi hii
   
 7. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,409
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Achana Nao hao MGONGO CHURA!
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  facebook customer care ingia homepage ya jf click tangazo lao hapo chini itaingia moja kwa moja facebook utakuwa umesha like page yao sasa wewe andika malalamiko yako dk 10 nyingi utajibiwa utapewa na email yao ya CC utatuma namba yako ya simu na wao watakupigia..

  asante kwa kujiunga na tigo tanzania on facebook
   
 9. K

  Kiwera Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi mwenyewe wameniibia laki moja kwa mtindo huu within 7 days.Nimekwenda ofice zao nachoambulia ni majibu yasiyoridhisha.
   
 10. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sio wewe tu, hata mimi nimenunua LUKU ya shs 10,000/= tokea juzi mpk leo sijapata chochote.Nmefuate taratibu zoote lakini hakuna chochote. Pia nimepiga hio 150 ndio wala haipokelewi. Nimeamu kuchukua uamuzi wa kuacha kutumia TIGO from now onwards.

  TIGO imejaa utapeli, ubabaishaji na wizi usio wa kawaida. From now onwards nahamia AIRTEL na VODA japo nazo sio bora sana.
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tigo mtandao wao hauaminiki juzi nilipiga simu kampuni moja nikawauliza ninunue kifurushi changu cha tv kwa tigo pesa au mpesa majibu niliyopewa kuwa tigo pesa inasumbua mpesa uhakika je ina maana hata hizi kampuni zinaingia mikataba na tigopesa bila uhakika!!!
   
 12. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Tigo ni majizi wakubwa,sitosahau walivyoniliza mchana kweupe..juzi tu hapa namtumia dogo pesa akamilishe tuition fee meseji kwangu wala kwake haifiki,dogo analia wamezuiliwa kufanya mtihan wa mwisho wa muhula mpaka walipe mkwanja..yaani ikabidi niingie gharama mara mbili kutumia benki,kuipata sasa hela yangu iliyopotea hewani ni ishu,kero nilizopata hadi nikiona nembo ya tigo kichwa kinauma..TCRA wako wapi watu wanaibiwa mchana kweupe!
   
 13. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Mimi nina afadhali, nimedanganywa ama kutapeliwa. Ukinunua luku kwa kutumia tigo pesa wanakwambia watakupa 10min za bonus. Lakini mimi leo nimenunua na sijiona hata sekumde.
   
Loading...