Watairudisha kama ndo tabia yao
Litafika hadi kwa Waziri ohooo
wezi sana hawa jamaa!
na kuna siku nyingine niligombana nao sana
nimenunua kifurushi cha sms cha mwezi nikawa na chat na shemeji yenu, cha kuskitisha baada ya kutuma sms kama 10 hivi , nikaona sms zinagoma
nikijaribu kutuma kwenda namba nyingine zinaenda, ikabidi niwapigie tigo kuwaeleza lile tatizo
walichonijibu , nikaona kweli hii kampuni hamna kitu kabisa
wakanambia sitakiwi kutuma sms nyingi kwenda kwenye namba moja
nikawauliza mnanipangia matumizi? kama ndio hivyo toeni elimu kwa wateja wenu wooote kwamba kifurushi chenu cha sms kina masharti kadhaa wa kadhaa ili mtu aamue ajiunge au asijiunge
sio mnakimbilia tu kukata pesa halafu unakuja kumpangia mtu matokeo, niligombana nao sana mwisho wakaja kuniachia nitume sms kama kawaida
kama kuna mfanyakazi wa tigo humu jukwaani wasilisha haya malalamikowaambie tumeshaanza kuwaandika majukwaani
sasa wasipokuwa makini tutafungua jukwaa special kwa ajili yao maana kero zimekuwa nyingi na hamzifanyii kazi