Tigo mnamdatisha binti yangu!!

Tigo mnamdatisha binti yangu!!

Unahangaika bure , mtoto mwenyewe siyo wako.

Kama unapinga nenda upime DNA
 
Mkuu wangu kama wako.Ana miezi 8 ila Pindua pindua linamchanganya sana.
hahaa mpaka wakwako kumbe ..daahh yaani haya matangazo ni research tosha yakutufnya wazazi tugundue talent za watoto wetu...kuna siku moja niliwahi kumsikia beyonce akisema alianza kuimba akiwa na miaka miwili nikaishia kuguna tu...lakini sasa hvi naamini
 
Unahangaika bure , mtoto mwenyewe siyo wako.

Kama unapinga nenda upime DNA
ha ha ha ; Mkuu una uhakika kwamba dingi yako ni dingi kweli??? Why don't you go and have a DNA test with him to confirm?
 
Mi wangu kadata na tangazo la BIKO....hasa pale mwisho wanaposema Biko mshiko nje nje......Hata kama alikuwa anacheza nje,akiskia tu,ataingia ndani kwa spidi ili awahi hayo maneno ya mwisho afuatishe wanavyosema....
 
Mwanangu Tatu akiona tangazo la EATV lenye robot anaetembea huku forever young ya jay z inalia na yeye anaanza kutembea Kama roboti..
 
Mimi wa kwangu akisikia sauti ya mapadlock anakuja mbio, uzuri mimi Nina klipu kibao nampatia anaendelea kwenye simu.
 
Mi mtoto wangu analipenda Sana lile tangazo la sabuni ya kuogea ya Revola.
Wadau nitalipata wapi tena lile tangazo?
 
Hilo tangazo sijui kwa nn watoto wanachanganyikiwa. Kituko kingine, kuna tangazo la fanta limeanza kurushwa hivi karibu mzee mmoja anajadiliana na vijana wake nani atabuni tangazo bora la Fanta. Vijana wanajaribu mzee anawambia wamekosea, mwishoni anajitolea kutengeneza mwenyewe, anakunywa Fanta kisha mdomo, masikio, macho yanambadilika yanakuwa kama katuni. My take-jana mtoto kaliona tangazo hilo lilipoisha akaniuliza inamaanisha nikinywa Fanta nitageuka kuwa katuni?. NASHAURI hilo tangazo rekebisheni halieleweki.
 
Mkuu naona umetumia mbinu kali sana kuleta tangazo la tigo......huu ndio ubunifu unaotakiwa.

Uzuri hapa huchajiwi chochote.
 
Mnaendekeza watoto wenu ujinga
Eti akililia kitu apewe
Mi ukilia unaongezewa vikofi....
Ukililia kitu hupewi labda kiwe chakula ila si simu wala rimoti
 
Mkuu binti yako lazima a takuja kuwa Mwigizaj
 
Mimi na utu uzima wangu nadata na sana na la "onjaa msisimkooo" sembuse ...
 
Kijana wangu wa miezi 8 akiliona hilo tangazo anafurahi sana lazima ainuke aanze kucheza
 
hahaa mpaka wakwako kumbe ..daahh yaani haya matangazo ni research tosha yakutufnya wazazi tugundue talent za watoto wetu...kuna siku moja niliwahi kumsikia beyonce akisema alianza kuimba akiwa na miaka miwili nikaishia kuguna tu...lakini sasa hvi naamini

Mamake alipokuwa na ujauzito wa miezi saba,alikuwa anaupenda sana ule wimbo wa Rockabye by Clean Bandit ft Sean Paul.Sasa ikawa kila mara anaupiga na na kuweka simu juu ya tumbo,basi dogo huko anarusha miguu balaa.Sasa alipozaliwa na kufikisha miezi sita tukawa tunaucheza,believe it or not,dogo akawa anafurahi na kupiga vikelele vya furaha.
 
Back
Top Bottom