Nimejaribu Modem ya Zantel, mwanzoni ilikuwa angalau afadhali kwa spidi, tangu walipopunguza bei imekuwa na spidi ya jongoo. PU****U kabisa. Hivi haya makampuni ya simu yamekuja kutuongezea umasikini? TCRA nao bomu pia. Wakati ule walisema tusajili simu zetu na simu ambazo zitakuwa hazijasajiliwa zitafungwa. Tukapanga foleni weeee, wakaongeza muda, baada ya hapo kimya kabisa. Watu wanapata matusi na vitisho kutoka namba ambazo hazieleweki kama kazi. RUSHWA IN ACTION TCRA??!!! Sasa oooh TV Digital mwisho wa Analog ni Desemba, Nawaambia hakuna lo lote litakalotokea, wanaleta usumbufu usio na maana. Nia yai ni kuvunja soko la nyungo za Analog tunazopata matangazo dezo. Hawastahili kusherehekea, kwa mafanikio gani? inaelekea hawajali malalamiko ya wateja. Wanaiangusha serikali ya JK.