Tigo mlichonifanyia sijapenda

Tigo mlichonifanyia sijapenda

lusheria

Member
Joined
Dec 2, 2016
Posts
8
Reaction score
1
Ndugu wanajamvi.

Mbarikiwe wote.

Tigo Tanzania sijapenda haya mambo yenu.

Leo nimenunua Salio katika tigo pesa ili nijiunge na huduma ya vifurushi. Mara gafla nashangaa naambiwa fedha yangu haitoshi kifurushi

Kucheki naona kweli Salio limekatwa. Ikabidi kupiga Simu huduma kwa wateja ndo nikastajabishwa kuwa nilijiunga na huduma ya "HADITHI NA SIMULIZI " na huwa nakwatwa hela iyo Mara kwa Mara . Nimeshangaa Sana .hizi HADITHI na SIMULIZI Mimi wapi na wapi ? Kwanza sijui hata zinaungwa vipi.! Au masimulizi hufanyikia wapi ? Simu yangu natumia ya tigo ni tochi.

Sijapenda kwakweli.

Nimekumbuka zamani niliwahi sikia jamaa mmoja wa bank alikua anakata sh.200 kwenye Kila hela ya mwalimu . Na sababu ili kuwa ndogo ilikuwa haionekani. Ila jamaa alifanikiwa kuwa tajiri. Nimehisi labda ni ka mchezo kanataka fanyika hapa tigo.
 
WANAKERA SANA, HILO HELA WANAZOPATA KWENYE VOCHA NA TIGO PESA HAZIWATOSHI??
 
Mimi nlikuwa nakatwa salio TTCL bila kujua kuna siku uzalendo ukanishinda nikapiga simu customer care nikaanza kuwa mkali kumbe mwanangu amachezea simu akwaweka imessage na facetime On kwny simu.

Ikabidi niwe mdogo tu na kuziweka off lkn nlikaa karibia wiki 2 bila kujua kwann salio langu linaenda tu na kifurushi cha mwezi hakijaisha
 
Pengine uliwasha data mkuu?

Hapa wengi tutumiawo SP huwa tunajisahau sana pindi tuongezapo salio.
 
Pengine uliwasha data mkuu?

Hapa wengi tutumiawo SP huwa tunajisahau sana pindi tuongezapo salio.

Mkuu line ya tigo ipo kwa tochi ... Na nimepiga Simu uko customer service wakasema makato ni sababu ya simulizi na hadithi .

Mimi sijawahi kujiunga Na hii mambo . Na nimeuliza hatua Za kujiunga ni hadi ujibu msg Yao ndo utapata iyo huduma.

Mbaya zaidi hata Izo SIMULIZI Na hadithi sijawahi kupigiwa wala kutumiwa maana ningeona lazma ningewapigia sababu najua zinakata hela .

Kwaiyo hapa kuna two coincidence... Nakatwa sababu ya simulizi na hadithi ambazo sijawahi jiunga. Pili sijawahi kupokea hizo hadithi Na memuuliza muhudumu anaona simulizi zimetumwa kwenye Simu yangu ya hizi hadithi akasema haoni....

Hii kitu ni Rahisi ivi kweli ..! [emoji848]
 
Binafsi sinunuagi tena vocha; airtime naifanya electronically, nafanya kama alivyo sema mleta uzi; kwa tigo natumia tigo pesa, Voda kwa mpesa nk; nikitaka kujiunga bando then naiunga ju kwa ju, sema tiGo huwezi jiunga bando la mwezi kwa tiGo pesa, nimegundua mitandao mingi tu, simu ikiwa na balance (airtime) wana kata tu so dawa ni moja, balance isome either 0 au less than Tsh 10, hapo hawana cha kukata
 
Dah itabidi nifanye ivi mana siwezi badilisha hii namba Iko kazini muda.... Ule utaratibu wa namba hii hii Ila mtandao mwingine sijui uliishia wapi ... Nitawahama kwa super sonic speed ..!
 
KWA MANUFAA YA WENGI, andika neno ONDOA kwenda 15668.utaondoka huduma zote ambazo umejiunga kwa kutokujua au kwa kuungwa na tigo
 
Dah itabidi nifanye ivi mana siwezi badilisha hii namba Iko kazini muda.... Ule utaratibu wa namba hii hii Ila mtandao mwingine sijui uliishia wapi ... Nitawahama kwa super sonic speed ..!
Halafu nadhani tiGo pia ni very expensive to operate with them though voda nao miyeyusho mingi, airtel walau wanajitahidi na hata bei zao zipo so reasonable kulinganisha na wengi.
 
Back
Top Bottom