Forforty
Member
- Nov 13, 2019
- 85
- 87
Salam wadau,
Ningependa niende kwenye mada moja kwa moja kwani nahisi kupasuka kwa hasira kwa upumbavu walionifanyia Tigo.
Nimekuwa mteja wa mtandao wa Tigo kwa miaka kadhaa sasa, ila nilichokutana nacho kama kitajirudia tena basi itakuwa mwisho wa mimi kutumia mtandao huu.
Ni siku ya tatu au ya nne sasa nimekuwa sipati sms za miamala ya Tigo Pesa pale ninapotuma au kutumiwa hata napoweka kibandani pia.
Lakini pia hata napofanya malipo kama kununua Luku inakuwa shida sana kupata sms ya Token mpaka napopiga simu huduma kwa wateja ndipo badae wananitumia sms ya Token, sio hivyo tu hata nikinunua vifurushi vya kupiga au internet pia sipati sms.
Leo pia imetokea mtu kanitumia hela sikupata sms, nami nikamtumia mtu hela pia sikupata sms ila niliyemtumia aliipata nikajiuliza mbona mimi sipati?
Nikatulia nikanunua Luku hela ikakatwa na sikupata sms mpaka muda huu navyoandika ujumbe huu na umeme ulikuwa umeisha nyumbani.
Nikamwambia tu wife anunue umeme tena kupitia kibandani kwenye mashine za Selcom ili mambo yaende.
Baada ya muda nikapiga simu huduma kwa wateja kuuliza kwanini sipati sms?
Nilichojibiwa ni kwamba sijaweka vicha ya kukwangua kwa muda hivyo inasababisha nisiweze kupata hizo sms, nikaambiwa nikiweka tu hizo vocha basi nitanza kupokea sms za miamala.
Baada ya kupewa majibu hayo nilipandwa na hasira nikanza kumuuliza maswali dada yule ambae hakuweza kunijibu hata swali moja zaidi ya kukaa kimya utadhani simu imekatika.
Maswali yalikuwa kama ifuatavyo:
1. Kwanini mliweka huduma ya kununua vocha kupitia Tigopesa?
2. Mimi kupokea sms za miamala ya fedha zangu mwenyewe inahusiana nini na hizo vocha za kukwangua?
3. Je wateja wenu wa Post Pay nao hawapati sms mpaka wakwanguwe vocha?
Kama ni kweli, nini maana ya hiyo huduma?
Nikamalizia kwa kumwambia dada yule awambie maboss wake waache ujinga msitulazimishe kununua vocha za kukwangua kibandani kwa mangi wakati mmeshatuletea huduma ya vocha kupitia Tigopesa.
Mwisho.
Tigo jiangalieni sana tambueni mnahudumia watu wengi na wengine wana uwezo kuliko hata nyinyi mliopo huko, acheni kuleta uhuni kama wa hawa manabii walioibuka awamu hii ya tano wanauza maji, mafuta na leso.