Tigo acheni uhuni wa darasa la pili B

Tigo acheni uhuni wa darasa la pili B

Ila speed yao ndo inazingua naona nnayo line ya chuo speed ndogo sana
Speed huwa inategemeana na signal za mnara husika. Mimi nastream sana hasa tv online kuangalia mechi za ligi ya ulaya iko poa sana.
 
Hawa jamaa wameanza kubana hata hela za matangazo. Matangazo wameweka kwenye calls. Yaani unampigia mtu hapatikani ila wanaanza kwanza kukupa matangazo lukuki bila mpango mpaka ikifikia point hapatikani ushapoteza dakika 2.

Asee tigo mnaboa toeni matangazo kwenye calls.
 
Ilinikuta ishu ya kama mleta uzi, nikawapigia akapokea mdada nikamueleze ishu akajibu huwezi kuunganishwa na huduma ambayo haujataka kujiunga. Nikamuuliza hapo ulipo unaona mimi nikiwa nimeomba kuungwa na hii huduma akajibu hapana, nikamuuliza sasa kwanini unang'ang'ania nitakua nimejiunga? Nikamuambia basi naomba suluhisho la hii ishu.
Akanielekeza jinsi ya kujitoa.

Lakini nikaja kugundua kua kuna websites hasa hizi za kudownload vitu zinakua zina clickbait, ukiclick inakupeleka kwenye page ya tigo vip na magemu kibao hujakaa vizuri ndiyo inaingia hiyo sms ya kama ya mleta uzi.
Ni kama ile clickbait wameifanya ukiibonyeza uwe umejiunga automatically, jambo ninaloamini pengine baadhi ya wafanyakazi wao hawajui (angejua yule dada angenielezea).
 
Leo nimepokea ujumbe huu kutoka Tigo. Wameniunganisha kwenye kucheza magemu na wanataka niwe nawalipa TZS.200 per day. Sijaomba waniunganishe na wala mimi sio mpenzi wa games.

Nimejaribu kutuma neno ONDOA kwenye 15302 ujumbe hauendi.
Jamani Tigo tunajua kuwa mmefulia kinoma na mnapunguza wafanyakazi wenu ili kubana matumizi. Tafuteni njia halali za kuongeza mapato yenu badala ya kuwa mnatusukumia shida tusizozitaka.
Sasa mmenipa ratiba nyingine ambayo sikuipanga, ya kutembelea ofisi zenu.
Hii ni gharama kuna nauli na gharama ya muda.
Tafadhali tuacheni tumechoka na wizi wa Taifa Hili, tuna majeraha ya kutapeluwa pesa tulizochanga Kagera na nyie tena mnatuongezea mengine
TUWACHENI TUPUMUWE
Maji ya shingo wamebanwa na Halotel hawapumui hao
 
Chonde chonde usije ukakopa tigo. Leo nikiwa naendesha kuelekea job nikiwa katikati ya maongezi simu yangu ikakata. Nikapiga ndipo kimashine chao kikarespond simu yako haina salio, bonyeza moja kupata sekunde 200 na utarudisha sh. 350/- Nikaona bora nibonyeze ili nimalizie maongezi. Nilipofika ofisini nikaongeza vocha ya tzs.5,000/- nikijua ntakatwa tzs.350/- Nikapokea ujumbe kuwa asante kwa kurejesha mkopo wako, umelipa tzs.5,000/- Unadaiwa tzs. 2,500/- Nikapiga simu customers service nikajibiwa eti hilo tangazo limekosewa, kwa namna Mimi ninavyo transact na tigo eti kiwango changu cha chini cha kukopa ni tzs. 7,500/-
Yani sijaridhika kabisa na utapeli huu. Kesho naenda makumbusho kwao vinginevyo tuonane mahakamani
 
Hawa tigo wafanyakazi wao hawana uweledi sijui wanatumwa..Mimi wameniunganisha kwenye upuuzi wao wa hadithi bila kuomba nilchoona cha msingi ni kuitupa line yao na kuamia Halotel..
 
Back
Top Bottom