Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 36,004
- 40,866
Naomba Tigo mfanyie kazi mambo yafuatayo na mje hapa kuuambia umma kwanini mnayafanya haya, na ni kwa maslahi ya nani hasa
- Mtu akinituma sms moja kwenye simu yangu, basi nitaendelea kupokea sms hiyo repeatedly siku nzima hadi inakera kuona inbox inajaa text messages zinazojirudia, mfano leo kuna watu kadhaa wamenitumia sms asubuhi, cha kushangaza mpaka saa hizi naendelea kupokea tens of text messages ambazo ni jumbe nilizozipokea asubuhi
- Nimepiga simu customer care several times naambiwa bonyeza 8 ili kuongea na mhudumu moja kwa moja, then zinafuatia several options, na ukichagua hizo options simu inakata, hili kwangu mimi naona ni usumbufu usio na lazima, kama mteja anashida ya kuongea na customer care, kwanini kusiwe na namba ya moja kwa moja badala ya kumpitisha kwenye hizo options zisizo na tija kwake (to me hizo bonyeza bonyeza ni kero na ni time wasters) kama shida yenu ni kutuwekea matangazo, basi mabango yenu yaliyopo barabarani yanatosha maana ni mengi sana na kila siku tunayasoma.
- Malalamiko ya wateja yanapotolewa mara nyingi yamekuwa hayafanyiwi kazi, kwa mfano niliwahi kuwapigia kuwaambia swala la bundle zenu kwisha pasipo mtu kupata huduma, limekithiri, kwa muda mrefu device inakuwa inasearch tu hata kwa saa nzima na hasa unapotuma au kupakua mafaili kwa email au whatsapp, kiuhalisia mnatupatia shida sana watumiaji na hasa mkituunganisha kwenye hivyo vifurushi vyenu ni kama mnatuibia, kama lengo lenu ni kutuonjesha huduma zenu basi boresheni kwanza mifumo yenu ndipo mtupe hivyo vionjo na siyo kutufanya specimen wenu wakati tunawalipa kwa kutaka huduma. kwakweli mnaboa sana ninyi watu!!