Tiger Woods aachana rasmi na mkewe

Ellin whatever her name is, is a golddigger period. If Tiger is/was a cheater she is/was a cheater 2. Hakuna anayefahamu nini kilimfanya Tiger afanye aliyoyafanya. Wanawake wakishaingia kwenye ndoa wanakuwa na viburi sana huyu ni mojawapo. Kama Tiger alikuwa hatendewi haki na mkewe mlitaka afanye nini? Kuachana haikuwa suluhisho la tatizo hasa ukizingatia kuna watoto Ellin alipashwa atafakari kabla ya kufanya maamuzi yeye anafikiri amepata deep down amepatikana atakula jeuri yake. Pesa ni matokeo unazo leo kesho huna asifikiri pesa ni kila kitu katika maisha. Tiger atarudi kwenye ulingo wa golf kwa kasi kubwa tu. The guy has been thru alot mwacheni awe huru..Go Tiger Go.
 
......Watoto watatunzwa lakini si kuendelea kuishi under the same roof na mume ambaye ni cheater.Nafuu Ellin ameamua kumdivorce Tiger.

Labda aamue kuishi bila relationship, lakini akiwa nayo tu ajiandae kuacha kila mwanaume atakayekutana naye maana kwa asilimia kubwa sana wanacheat.
Kikubwa kwa wanandoa ni kusameheana, na kama alishamuomba msamaha si amsamehe tu? labda kama alikuwa na sababu zingine na penzi lilishaisha, so ni kama kapata sababu
 
lakini inafanana na ile ya Ashley na Cheryl Cole, kwani inaonekana woods ndiye mwenye matatizo. katika miezi ya hivi karibuni woods alijipa likizo ndefu kwenye mechi zake za gofu ili kumwangilia ndoa yake lakini sasa kama wamefikia hatua hiyo ni wazi huyo bibie atakuwa ameshindwa kumsamee tiger kama cheryl alivyoshindwa kufanya hivyo kwa mumewe, mwana kabumbu ashley cole.

Ukisema wote Tiger na Elin wana matatizo ntakukubalia. Ila sio kumbandika makosa Tiger moja kwa moja inabidid uangalie "profile" zao.

Ila upo sawa unapolinganisha kesi yao na ile ya akina Ashley na Cherly Cole. Walikuwa wakiishi kwenye jengo lenye apartments pale London bila ya kufahamiana Ashley akichezea Arsenal na Cherly akiwa mwimbaji kwenye kundi la Girls Aloud.

Mwimbaji mwenzie Cherly aitwae Kimberley Walsh nae alikuwa ana "boyfriend" ambae alikuwa akichezea Arsenal na Ashley kwahio Kimberley akatoa namba ya simu ya Cherly kwa Ashley na yeye kufanya utaratibu wa mawasiliano na baadae kumpata Cherly hio ni mwaka 2004. Hawakukaa sana wakachumbiana mwaka ulofuata na mwaka 2006 wakaoana.

Lakini baadae maisha ya ndoa yakawa magumu kwa watu hawa Cherly akiwa busy na safari za kuzunguka sehemu mbalimbali kutumbuiza na muziki (music tour) na pia kushiriki uamuzi kwenye kipindi maarufu cha X- Factor. Ashley akawa yupo "busy" anakutana na mabibi kwenye hoteli mbalimbali London (kumbuka alipokwenda Chelsea alikuwa akilipwa paundi 90,000 kwa wiki) na wakti mwingine alikuwa akishiriki "roasting sessions" (hii nafikiri utaelewa).

Haya mambo ya "cerebrities" kama hawa yanafaa kuwaachia wao wenyewe kwani wao ndio waamuzi wa lolote litakalotokea. Wanapenda "headlines" picha kwenye magazeti na maisha yao yanaendeshwa na "media" na ni hizi media ndizo zinaweza kulinda au kubomoa ndoa za watu hasa kama wewe una pesa na unafanya mambo mengi ya ajabuajabu.
 
......Watoto watatunzwa lakini si kuendelea kuishi under the same roof na mume ambaye ni cheater.Nafuu Ellin ameamua kumdivorce Tiger.

apart from kwamba ni goffer number one duniani,there is something serious wrong!!!jamaa anakiusaiko fulani.ukisikiliza mazungumzo yake unaona kabisa kuna kitu kina miss.bora dada wa watu kapata kimshiko chake na kaanza watoto watakua tu,kuna faida gani ya kulea watoto bila amani ,upendo na furaha.
 
WomanOfSubstance THE, masharti yakivunjwa ufanyeje, ulegeze masharti? Na unajuaje hawakuwekeana masharti na yakavunjwa?

Wanawake wa Kitanzania ni kama kondoo, mmefundishwa kuvumilia na kusamehe kila uchafu na ushenzi wa mwanamme, unaambiwa fia kwenye ndoa. Mfumo dume. Mzuri maana unatunza ndoa ila unaishi kwenye shurba na mateso.

maneno mazito hayo, ukweli kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom