Tido Mhando awa bosi Al-Jazeera Kiswahili!

this is very gud. hii ishu ya meremeta na fisadi General Shimbo inabidi Bwana Tido aimulike kisawasawa. mpaka hawa magamba yaogope. maana wamezoea kuigeuza nchi ye2 shamba la bibi
 
Ni kweli hata mm ungekuwa muda wangu wa kuwaanika hawa magamba kila siku dunia nzima iwajue,sasa hapa watz watalaamu wetu wakigoma kurudi akaamua kufanya kazi nchi za wenzetu tutawalaumu?????hapa fitna nyingi.
 
News alert: si kweli kuwa dunstan tido mhando kachukuliwa na al jazeera.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Bw. Dunstan Tido Mhando, hajachukuliwa na Al Jazeera, kituo cha habari cha kimataifa chenye makao yake mkuu jijini Doha, Qatar, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha.Uchunguzi wetu wa kina kufuatia habari hizo kuchapishwa katika mitandao ya jamii kwa muda wa wiki mbili sasa unaonesha Al Jazeera sio tu hawajamchukua Tido bali pia yeye mwenyewe hajaomba kushika wadhifa huo. Vyanzo vyetu vya habari vilivyo karibu kabisa na Tido vinasema yeye mwenyewe ameshangazwa na uvumi huo ulioanzishwa na mtandao wa Jackal News wa nchini Kenya kwamba Tido Mhando na Joseph Warungu, maveterani wa BBC, wamehamia Al Jazeera.Vyanzo hivyo vimehoji kwamba Al Jazeera kikiwa ni chombo makini cha kimataifa kisingekuwa na haja kutangaza hadharani nafasi za kazi kadhaa ikiwamo hiyo ya Ukurugenzi wa idhaa yake mpya ya Kiswahili katika Afrika Mashariki endapo kama wangekuwa wameshampata Tido.Vimesema vyanzo hivyo kwamba hivi sasa Tido yuko mbioni kufungua kampuni yake binafsi na wala hana mpango wowote wa kwenda Al Jazeera ama chombo kingine chochote."Endapo kama vyombo vilivyovumisha mambo haya vingekuwa makini vingemfuata Tido mwenyewe kujua ukweli wa mambo," vimesema vyanzo vyetu vya habari.Tido, ambaye alimaliza mkataba wake na kuondoka TBC mwishoni mwa mwaka jana, amekuwa hasikiki na mara ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa wiki mbili zilizopita kwenye msiba wa mke wa Mzee Mikidadi Mahmoud. Juhudi za wanahabari kutaka aongee siku hiyo hazikuzaa matunda.Leo Globu ya Jamii imeweza kuongea na Tido Mhando, naye kathibitisha kwamba yuko njia moja kufungua kampuni yake binfasi, ambayo hakuitaja jina wala kutoa tarehe za kuanza kazi na kazi aina gani. Naye alionesha kushangazwa habari zinazomhusu yeye kuhamia Al Jazeera na kukataa kuongelea kitu alichokiita uvumi usio na ukweli.Globu ya Jamii pia ilizungumza na mratibu wa nafasi za kazi zilizotangazwa kwa idhaa yake mpya ya Swahili Service, naye kaoneshwa kushangazwa nan habari hizo, akisisitiza kwamba si rahisi wao kutangaza nafasi ambayo keshapewa mtu
SOURCE: MICHUZI BLOG
 
Fundisho kwa wengine,Mungu si mwanadamu na ukifika huko sijui watakufanyaje,naamini roho iko juu watu ni bora aombe apate kazi ili akatimize ndoto
 
Back
Top Bottom