Ticts kupewa mkataba mpya?

Ticts kupewa mkataba mpya?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,110
Pamoja na utendaji mbovu bandarini na malalamiko mengi kuhusu makusanyo ya fedha bandarini na utata wa mkataba wake serikali imeiongezea kampuni hiyo mkataba wa miezi 3 wakati ikiendelea na mazungumzo.

Je huu sio wakati muafaka wa serikali kutafuta mwendeshaji mwingine mahiri ambaye ataongeza mapato ya bandari?

Kwa nini wahusika bado wanaikumbatia hii kampuni pamojana utendaji mbovu?

swahilitimes-___2943042521370589939___--1.jpg
 
Unamuondoaje Rostam Aziz na JK Bandarini?

si kweli, mwenye chaka lake bila shaka ni marehemu na walikuwa wako na jamaa mmoja wa midizini huko.

kwasasa fupa linawaniwa na wengine maana jamaa wa midizini hana nguvu na mwenye miguvu marehemu tayari, RA na BT hilo halikuwa chaka lao aka kitengo chao.
 
si kweli, mwenye chaka lake bila shaka ni marehemu na walikuwa wako na jamaa mmoja wa midizini huko.

kwasasa fupa linawaniwa na wengine maana jamaa wa midizini hana nguvu na mwenye miguvu marehemu tayari, RA na BT hilo halikuwa chaka lao aka kitengo
 
Ticts nashauri apewe tu mkataba japo kuna mazingira ya upigaji lakini wanafanyakazi kubwa tofauti na TPA. Wana vifaa na wanaheshimu wafanyakazi wao.

Moja ya shareholder wa kubwa ambaye alikuwa akiwakilishwa na karamagi ni RA. So RA unaweza kumnyanganya mgodi wa baharini kirahisi kweli with all his lobbying skills and connection. Ashakuwa mweka hazina wa chama huyu. Ashamiliki vodacom, sasa Tigo ambayo inamiliki zantel, Caspian mining and Construction huyu muajemi ni kama mhimili uliojichimbia chini zaidi.

Juzi mwanae kaoa wadau wote wa nchi wameenda kula ubwabwa na shehere imeisha wakapewa na bahasha.
 
Back
Top Bottom