Ticts jobs | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ticts jobs

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Jaxx, Apr 22, 2011.

 1. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF kwani nitangulize shukrani zangu kwa ushirikiano weenu wa kila cku, nitakuwa tofauti kidogo na hisia zenu kutokana na heading ila lengo ni moja tu kusaidiana maisha maggumu kama hayo
  Kuna kampuni Inaitwa Lukundo Co. ltd ni agent wa TICTS hapa bandarini kitengo cha uhakiki wa mizigo yani Tallying, Bahati nzuri jamaa (Lukundo) walitangaza kazi za Tallying Clerk nikaomba na nikapata japo pia zoezi lilitawaliwa na Rushwa,chakushangaza na kilichofanya ni post hii thread ni kuwa leo yani tarehe 22/04/2011 tuliambiwa tuanze kazi na mpaka hapo tukawa hatujaambiwa mshahara ila mbaya zaidi mimi nimefukuzwa kazi eti KISA nimeuliza mshahara ni kiasi gani?, hivyo nimepoteza kazi na wote zaidi ya 80 walioajiliwa mpaka sasa wameanza kazi ila hawajaambiwa mshahara ni kiasi gani na hakuna mkataba, eti hili ndilo soko la ajira,Mtu anaeenda kufanya kazi ya kuidhinisha na kukagua mizigo ya Billions of shillins anaanza kazi bila mkataba wala kujua mshahara?, ni hatari sana hivyo TICTS kuweni macho sana na hizi kampuni mnazozipa kazi
  Naomba kuwasilisha!!!
   
 2. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Pole sana mkuu.
   
 3. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  pole sana. Hii ni muendelezo tu wa uozo katika taasisi nyeti katika utamaduni wa kuendekeza njaa. Kwa mtindo huo si ajabu wizi, ubabaishaji, ucheleweshaji kuendelea pale TICTS. Kila siku wanatangaza kazi utadhani wanapeleka watu Iraki. Duh!
   
 4. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana kichwat
   
 5. s

  sirmudy JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  pole sana kaka, ndo majaribu ya dunia. ila kwa vile una elimu yako just wait,post zingine zikitoka omba , na sio lazima ktk kampuni hiyo, kampuni ziko nyingi. Achana hao mafisadi wa bandarini. Ni haki yako kujua mshahara wako and other benefits kabla ya kuanza kazi, ila hao 79 waliobaki hawalijui hilo na wataendelea kuburuzwa hadi watakijua.
   
 6. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu duh tunangia mkenge kwa sababu ya soko la ajira kuwa dogo.
   
 7. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Pole sana mwanaharakati.Siku zote mpenda haki hapendwi.Tafuta kwingine utapata hakuna wasi.
   
 8. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana
   
 9. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante mkuu hayo ni mapito tu
   
 10. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamekuta kazi na si vyeti wala cv yako.Fighter never give up kaza buti utapata kwingine.Duh,pole sana mkulu.
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Inaonesha hio kazi ni uzushi tu, jamaa alobaki hapo kama yuko passive ili tu aishi hapa mjini imekula kwake. Pole Jaxx utapata kazi nyingine.
   
 12. c

  corleone Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole, utapata kazi nyingine.
   
 13. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Hicho ni "kibarua". lolz
  HAWANA HADHI WALA UWEZO WA KUKUAJIRI!
   
 14. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakin hata kibarua huambiwa ujira wake wa kila cku anayofanya kazi
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  LUKUNDO CO LTD lazima itakua kampuni ya wapare hiyo!wamepitia kwa karamagi
   
 16. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  TICTS? .......Nilijua tu! Hawa si ndo wale walisainia mikataba yetu gesti ughaibuni? Hawajua umuhimu wa mikataba. Hata kama ni mawakala wao lakini wote ni wamoja.
   
 17. F

  Ferds JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pole mkuu, ila hilo si la ajabu ktk makampuni binafsi , wenyewe wanasema kuwa ktk secta binafsi hakuna security of employment, kuna mtu hapa nianpofanyakazi alifukuzwa na GM(general manager) kwa kukutwa anasoma gazeti maeneo ya kazi, sasa watu wanajiuliza inamaana hutakiwi hata kupozi kidogo , yaani hapa hata hiyo lunch tunayoenda tunaambiwa kukompaset, yaani ule mda wa kawaida wa kutoka umeongezewa 30minutes za lunch, sasa imagine!! huu ndio uwekezaji tunaoukumbatia

  • :frusty:
   
 18. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  pole mkuu utapata kwingine,huo ndio ufisadi
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ferds; mbona wa kusurf na kupost unao? Jamani kuweni wakweli saa nyingine. Sisi wa TZ wakati mwingine tumejijengea tabia ya uvivu au ya kujivuta na mtu akiwa makini kuhakikisha mtu analipwa haki yake (unalipwa ulichofanyia kazi) tunalalamika.

  Jaxx kwa ishu ya LUKINDO pole, labda wamekugundua kuwa ulikuwa si mfanyaji kazi labda ulijipenyeza kuwachunguza kama inavyoonekana!!!
   
 20. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Ufisadi tu mkuu nchi hii,ipo siku.
   
Loading...