TIC, TAN-TRADE, EPZA, TTB & BRELA: Mrundikano wa Taasisi zinazofanya kazi zinazofanana

watuache hivi hivi taasisi zikiwa nyingi hata watu tunapata vyeo (posho, magari V8 na dili za procurement)angalau mtu unaweza jenga nyumba zako kadhaa za kupangisha. mishahara yenyewe midogo
 
To me ni namna ya kucreate ualaji serikalini tuu hamna kingine.
Mwisho wa siku wanatupiana mzigo kwenye kutelekeza majukumu yao.
 
Nimekaa nikafikiri hapa TZ tuna taasisi nyingi za Serikali kuanzia Tanzania Investment Centre (TIC), EPZA, Tanzania
Tourist Board (TTB), TAN-TRA, BRELA etc. zote zinafanya kazi almost sawa na sioni logic ya kuwa nazo zote. Ningependekeza iundwe Kampuni/Mamlaka mfano: BRAND TANZANIA AUTHORITY halafu hizi taasis ziwe idara ndog ndogo chini ya hiyo mamlaka katika kubana matumizi na kuongeza ufanisi. Vinginevyo kuifanya Tanzania Middle Income country by 2025 itakuwa ni ndoto.

Ungeuliza tofauti ya hizo organizations ni nini?

TTB haileti investors bali iko busy na watalii, TIC haifungui export processing zones bali inafacilitate invenstors kwa sera na mazingira wezeshi, BRELA ni kitu kingine tofauti kabisa, same kwa TAN-TRA

Sevu muda kidogo, nenda google, pitia organization moja baada ya nyingine, halafu kwa kukusaidia tu, chora jedwali uwe unaorodhesha kwa kila organization vitu vifuatavyo: mision, vision, malengo/objectives, kazi zao za msingi, wadau wao wa karibu na baadhi ya mifano ya mafanikio yao.

Ukikuta kama wameweka na strategic plans zao pia summarize

Ukimaliza uje na mrejesho
 
janjaweed! nyie ndo mizigo ya nchi hii, rudi shule ELIMU ni BURE kwa sasa, katika muendelezo ule ule wa kubana matumizi taasisi tajwa (zote) zinaweza kuunganishwa na kuwa na taasisi na idara kadhaa.
 
1. NIDA - Vitambulisho,
2. Tume ya Uchaguzi - Vitambulisho,
3. Immigration Dept. - Passport=vitambulisho
4. TRA - Leseni/kitambulisho
5. PPF/NSSF, GEPF n.k - Vitambulisho.
 
Taasisi za elimu zinazofanana nazo ni kero;
1. Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam. DIT
2. Chuo cha ufundi Arusha, ATC,
** Changanya pamoja, Mkuu wa Chuo awe mmoja hiyo ya Arusha iwe tawi/campus ya DIT
 
tufike mahala serikali ipunguze hizi gharama za kuwa taaasisi lukuki za kufyonza pesa za mlipa kodi na tija ikiwa ndogo mno
 
Nimekaa nikafikiri hapa TZ tuna taasisi nyingi za Serikali kuanzia Tanzania Investment Centre (TIC), EPZA, Tanzania
Tourist Board (TTB), TAN-TRA, BRELA etc. zote zinafanya kazi almost sawa na sioni logic ya kuwa nazo zote. Ningependekeza iundwe Kampuni/Mamlaka mfano: BRAND TANZANIA AUTHORITY halafu hizi taasis ziwe idara ndog ndogo chini ya hiyo mamlaka katika kubana matumizi na kuongeza ufanisi. Vinginevyo kuifanya Tanzania Middle Income country by 2025 itakuwa ni ndoto.
Kwa maana nyingine ni sawa na kusema tuivunje IMF na WB tuunde kitu kimoja kwa maana hata hizo zinafanana majukumu
 
Tunakoelekea Huko mtashauri hata shule za msingi na secondari ziunganishwe na Kuwe na shule moja tu Tanzania nzima.
Point yangu iko pale pale, taasisi moja Kubwa is un manageable na inakuwa na ukiritimba. Moja ya Njia ya kuondoa ukiritimba na kuleta ufanisi ni kuvunja na kutengeneza multiple organization Amazon zitashindana zenyewe kwa zenyewe na hi yo kuleta ufanisi. Nafikiri mnaona minis sasa hivi jinsi mifuko ya jamii inavyo chacharika.
Hapa nakukubali ila si kwa hii mifuko ya jamii iliyolundikana
 
Inashindikana nini Taasisi kama NIDA ambayo inafanya kazi zinazofanana kabisa na RITA kuwa taasisi moja?
 
Ukitaka maendeleo halisi ni lazima taasisi za uzalishaji ziwe nyingi dhidi ya zile za usimamizi.
Kama wasimamizi ni wengi kuliko wazalishaji, maendeleo yatakuwa ya kinadharia tu. Ni lazima uzalishe kwanza ndipo upange na kusimamia matumizi ya kilichozalishwa.
 
Lesabu11 umezungumza jambo la maana mno. Fikiria hata vyu vikuu vyetu vinatoa kozi za kuwafanya vijana wasubiri kuajiriwa (wasimamizi) badala ya kuwapa maarifa ya kuzalisha.
cc. TEKU, MUM & SAUT.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom