TIC: Ajira 70,000 kuzalishwa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TIC: Ajira 70,000 kuzalishwa nchini

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Nov 28, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]Monday, 28 November 2011 10:46
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]Exuper Kachenje
  KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesajili miradi 735 ya uwekezaji nchini inayotarajiwa kuzalisha ajira 70,000 kwa Watanzania hasa vijana ikitarajiwa kuliingizia taifa Sh118 bilioni.

  Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu hali ya uwekezaji nchini kati ya Januari hadi Novemba mwaka huu , Meneja Uhusiano wa TIC, Pendo Gondwe alisema kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuliingizia taifa dola 6554 za Kimarekani, sawa na takribani Sh118 bilioni za Kitanzania.
  "Hali ya uwekezaji kwa mwaka huu ni nzuri. Kati ya Januari hadi Novemba TIC imeweza kusajili miradi 735 na tunategemea itazalisha ajira zaidi ya 70,000," alisema Gondwe.

  Alifafanua kuwa ajira hizo 70,000 ni ongezeko la ajira 26360 ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo kupitia miradi ya uwekezaji zilizalishwa ajira 43640.

  Alisema kuwa kusajiliwa kwa miradi hiyo ni ongezeko ikilinganishwa na miradi 509 iliyosajiliwa mwaka 2010 ambayo iliyokuwa na thamani ya dola 5066 milioni za Marekani sawa na kiasi cha Sh92 bilioni za Kitanzania.

  Alibainisha kuwa miradi inayoongoza kusajiliwa ni pamoja na ya utalii ni 198 ikifuatiwa na miradi ya viwanda ambayo ni 186 huku ile ya usafirishaji ikiwa 115 ikishika nafasi ya tatu.

  Gondwe alisema katika miradi hiyo iliyosajiliwa mingi wawekezaji wake ni wa ndani ambao alisema wamewekeza katika ujenzi wa majengo ya biashara, utalii na kilimo.

  Alisema TIC imeweza kusajili miradi hiyo mbali na mtikisiko wa uchumi duniani uliotokea mwaka 2009.

  Kuhusu ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkakuzi wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kituo hicho, Gondwe alisema kuwa TIC imekuwa ikipata hati safi miaka yote akitoa mfano wa mwaka 2009/2010 na mwaka 2010/2011.

  Alisema kwamba kwa miaka hiyo CAG alitoa hati safi ya ukaguzi wa hesabu kwa kituo hicho akinadi kuwa hapakuwa na taarifa wala hisia za ubadhirifu wa fedha au ufisadi.

  Alisema kufuatia TIC kupata hati safi, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Poac), ilitoa maelekezo na ushauri uliokuwa na nia ya kujenga.


  MY TAKE:

  Mwaka mzima wamefanikiwa kusajiri miradi 735 ambayo itaajiri watu takribani 70,000 which means kila mradi utaajiri watu 95.
  Ninaanza kujiuliza aina ya iyo miradi isije ikawa ni ile ya wachina kuuza maua bse uwiano wa miradi na waajiliwa ni mdogo sana.Hii inanipa picha kuwa TIC wako bize na vimiradi uchwara bse by now with more graduates in the market izo figure ni peanut.
  TIC kaeni na Serkali mje na mikakati endelevu ya kuwaajiri vijana ambao wako lundo mtaani kwa kufuatilia kwa umakini hii miradi ina wageni wangapi na watz wangapi?
  On the other hand uhamiaji mtusaidie kuwaondoa hawa wanaokwiba ajira za watz kwa kuanzia muanze na hawa wakandarasi wanaleta mpaka madreva wa kuendesha tipper kutoka India na China why?na wanapitaje Airport?
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu hawa tic ni usanii tu, c mara ya kwanza kusema kuna miradi itazalisha ajira kadhaa.
  - hao wawekezaji nao ni usanii wa kufa mtu, unakuta kwenye proposal zao wanadai wataajiri watu 100 halafu wanaishia kuajiri 50,

  - na hapo hata kama zipO mkuu nyingi ya hizo c za profesional, utakuta unskilled labour na miradi mingi kuachilia hiyo ya migodi, nyingine nyingi za za viwanda vya wahindi wetu na nazani unawapata hawa wahindi wetu kwenye swala zima la ajira.

  - NA HATA HIZO ZA UNSKILLED LABOUR BADO UNAKUTA KUNA WATU WAMESAFIRISHWA KUTOKA PAKSATAN NA INDIA KUJA KUFANYA HIZO KAZI.
  - CHEKI HATA HAWA WACHINA WANAO JENGA BARABARA UTKUTA YALE MAGREDA YANAENDESHWA NA WACHINA KUNA HADI MADREVA WA MAGARI YA MICHANGA WACHINA.

  - au utakuta ajira zile nzuri zote wanapewa watu kutoka nje wabongo wanaambulia ajira zenye mshahara mdogo sana. Mfano
  - ulinzi
  - usafi
  - kupanga mabox kwenye magodown
  - madreva
  - secretary

  ila ajira nyingi nzuri hata huku arusha kwenye makampuni ya utalii zinakamatwa na wazungu, wakenye, wahindi, na waganda,
  - kazi kama za uhasibu
  - hr
  - meneja
  - it

  hapo wa kulaumiwa ni serikali, na uhamiaji wao no vinara wa kufanya haya. Na kuna mtu aliniambia uhamiaji huwa wana ahidiwa mpaka nafasi nzuri za kazi kwa watoto wao na ndugu zao that is why wanafumbia haya
   
Loading...