TIBAIJUKA: Lazima wa TZ mlipigie Coco Beach

Juzi nilikua hapo coco napata moja baridi. Nikatoka na kupata muhogo pale kwa pembeni. Akaja binti anadai malipo ya parking sh 1000!! Kidogo nimtoe roho! Maana hasira zooote za dowans,mgao,uchakachuaji wa kura n.k. nilihamisha kwake!
 
nchi ishauzwa hii...... hlo swala la kulipia maegesho pale coco hata mi lilinikera sana...... yani unaweza ukapata dhambi ya kuua kutokana na tamaa za wa2 flan hivi......
 
Nalipia elfu 1 ya nini? Ni huduma gani wanayonipa in exchange for me parking there? Ardhi ya nani ile? Basi watu watalipa hadi kuogelea! Sehem yenyewe chafu na hata ingekua safi sitegemei kua hela ya parking isafishe wakati mijitu inakula hela tu huko juu.
 
Sijaelewa kulipia Parking au kapewa hilo eneo mtanzania kuliendeleza ili watu wakija kule wakute madhari ni nzuri kwa malipo walipayo waendapo kupumzika au malipo ya parking?

Na kwanini hilo tamko litoke leo kunani nyuma ya pazia???? wanamtafuta mchawi au?? maaana nchi hii usikute mtu alisha nunua hilo eneo jamani na ndio maana watu wakaambiwa walipie au? Imekuwaje kuletwe ufafanuzi hapo juu ya hili swala
 
hata kama ni kulipia kwa nini iwe 1000, na hakuna security wala nini, imeniuma sana nilipokuwa hapo xmass, lakini sikulipa
 
kwa nini hawa jamaa wasiuze vile viwanja vya ikulu ambapo wanasema kuna zoo na badala yake wanafuga bata mzinga tuu.
 
Hivi kwanini kama ni mradi halali wasitoe tangazo may be a month before waone reaction ya wananchi. Hii ingewawezesha kujua ni jinsi gani yakuwaelewesha na taratibu gani zinakubalika kwenye huo mpango wao. Kitu chochote hata kama nicha maendeleo ni lazima ufahamishe watu kwanza sio kushtukiza kwasababu support ya wananchi ni muhimu sana. Kinyume na hapo watu wanakuona we ni muhuni tu.
 
kabla ya kuanza kulipisha wangepaboresha kwanza na kupafanyia usafi..kwa sasa tunalipa for wht? even that 1000 it iz too much at least 500.
 
Back
Top Bottom