Tiba ya kunuka miguu

Tiba ya kunuka miguu

Mshkaji wangu ananiaga ananiambia leo sirudi home we funga tu mlango.

Hiyo ilikua ni saa mbili usiku.

Saa nne usiku ananipigia simu. Namuuliza mbona umenipigia usiku haufanyi kazi? (Nikimaanisha hamegi) akajibu 'Nipo nje'
Nikauliza kwanini akajibu 'Tumeingia ndani nimevua viatu kasema miguu yangu inanuka so nikae nje hadi iwe poa ndo narudi'

Nilicheka sana.
 
Awali ya yote nichukue nafasi hii kuwapa pole sana wale wote wenye hili tatizo asilimia kubwa wakiwa ni wanaume.

Ni tatizo linalokera na kufedhehesha sana, hivyo kuwanyima wengi raha na kukosa kujiamini.

Hili tatizo lina viashiria na vyanzo vingi lakini ukiachana na lile tatizo linalowekwa kwenye kundi la magonjwa ya ngozi kutokana na maambukizi ya vimelea vya bakteria na fungus, kuna chanzo kingine kisichopewa kipaumbele na wengi! Nacho ni uchafu, jasho na kutosafisha vizuri miguu.

Wengi wetu ni mabingwa wa kuoga kwa kumwagia maji na kupaka sabuni na kujisuuza bila kujali sehemu muhimu za maungio na viungo vilikobanana. Maeneo haya ni muhimu kupewa usafi wa pekee ama wa ziada.

Kwa mfano vidole miguuni licha ya kuoga mwili lakini ni muhimu sana kumalizia kwa kusafisha kwa makini sehemu zote katikati ya vidole.

Kisha zingatia yafuatayo:-
1. Vaa soksi safi
2. Vaa soksi kavu
3. Usirudie soksi
4. Usivae soksi kavu lakini miguu ikiwa na unyevu
5. Epuka kuvaa viangu vya plastic ama ngozi bandia
6. Kumbuka kusafisha viatu kila mara
7. Epuka kuvaa viatu vyenye unyevu
8. Zingatia kuvaa viatu na soksi vinavyoruhusu hewa kupenya nknk

Kama tayari una hili tatizo ufanyeje?

Wengi wetu hukimbilia hospitali ama kutumia marashi kuua harufu lakini hapa unaongeza tatizo badala ya kutatua.

Fanya hivi:-
1. Hakikisha miguu yako inakuwa safi katikati ya vidole kabla ya kulala na hata baada ya kulala
2. Tumia mchanganyiko wa maji yenye ndimu na chumvi kusafisha miguu mara mbili kwa siku
3. Tumia mafuta ya nazi halisi kupaka katikati ya vidole mara mbili kwa siku..
4. Hakikisha muda wowote unapovaa viatu miguu vidoleni ni safi na mikavu, soksi ni safi na kavu na viatu ni visafi na vikavu...

Utakapofanya yote haya na bado tatizo liko palepale wahi hospitali kwa uchunguzi zaidi na tiba
sie wa mkoani tuna comment wapi maana hayo maelekezo ya wanaune wa DAR
 
Mshkaji wangu ananiaga ananiambia leo sirudi home we funga tu mlango.

Hiyo ilikua ni saa mbili usiku.

Saa nne usiku ananipigia simu. Namuuliza mbona umenipigia usiku haufanyi kazi? (Nikimaanisha hamegi) akajibu 'Nipo nje'
Nikauliza kwanini akajibu 'Tumeingia ndani nimevua viatu kasema miguu yangu inanuka so nikae nje hadi iwe poa ndo narudi'

Nilicheka sana.
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji848][emoji848][emoji23][emoji23][emoji23]inachekesha lakini inaumiza pia
 
Aisee sisi wa site ndo hali tete sana, unavaa safety boot mchana joto kali kweli,
Ila Mimi sinuki miguu kaka[emoji28]
 
Kwa kuongezea jaribu kuwa na pair zaidi ya moja ya viatu ili uweze kuvipumzisha na kupata hewa safi
Wengine wanafanya kazi za site n wapo site siku zote za Juma, wakipewa pair moja ndo hiyo hiyo anakomaa nayo miezi 6 , 8 au mwaka,
Ila nitashauri jambo kazini kwangu
 
Pair mpya ya socks ni muhimu kuliko chupa ya bia
Soksi mia tano mpaka elfu.
beer elfu mbili mia tano hadi elfu tatu hala beer lazima unywe kwa uchache sita ili upate ka steam.
Sijataja kongoro na vocha ya mchepuko.
Lkn hatununui soksi
 
Back
Top Bottom