Thobias Kifaru: Kiongera, Kwizera ni wauza mitumba

Thobias Kifaru: Kiongera, Kwizera ni wauza mitumba

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
2,949
Reaction score
1,943
INAONEKANA ushindani wa Ligi Kuu Tanzania Bara umekuja mapema hata kabla ya muda wake, sasa ukitaka kuamini sikia kauli hii iliyotolewa kutoka Mtibwa Sugar kwenda kwa Simba.

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amesema kuwa Simba haijafanya usajili wowote wa maana na ndiyo maana inaogopa kucheza mechi ya kirafiki dhidi yao.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni baada ya Simba kukataa kucheza na Mtibwa katika mchezo maalum wa kufanya majaribio ya tiketi za kielektroniki, uliokuwa upigwe leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kifaru alisema Simba waliogopa muziki wao kwa kuwa usajili wao hauna lolote na kudai kuwa wachezaji wao wapya wakiwemo Paul Kiongera na Pierre Kwizera ni sawa na wafanyabiashara wa mitumba na siyo wachezaji hatari.

"Mtibwa siyo timu ndogo ndiyo maana Simba wameogopa, hao wachezaji wao wapya ni wauza mitumba. Mimi siamini kama ni wachezaji wa kimataifa. Wanatudanganya tu, wanatuletea watu wa mitaani, wanasema ni wachezaji," alisema kwa kujiamini.
Simba, imepanga kujipima dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini.


Chanzo: GlobalPublishers
 
Kwani muuza mitumba akiwa anajua kucheza mpira hadi akachaguliwa timu ya taifa kuna tatizo gani?
 
Kama Tobias Kifaru anamaanisha anachokisema, swali ni je, kwanini Mtibwa waliomba wacheze na timu yenye wachezaji wauza mitumba?
 
Ana maneno ya ngomani tena ya kizaramo wauza mitumba wanachezea timu yao ya taifa,asubir ligi ianze ndio aseme hayo maneno yake.
 
Nahisi kuna ukweli fulani kwenye kauli ya Kifaru.
 
Timu nzima ya Ashanti na washabiki wao ni WAUZA MITUMBA
 
Back
Top Bottom